Rosemary Senyamule Rc Dodoma
NA JOHN BANDA, DODOMA
UTAFITI wa Kilimo na Uchumi uliaonza kufanyika mwishoni mwa mwaka jana unatarajiwa kukamilishwa ndani ya miezi miwili Mkuu wa mkoa wa Dodoma akiwataka wananchi kutoa ushirikiano wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo.
Akiongea leo Januari 15,2024 ukumbi wa Ofisini yake na Waandishi wa Habari, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema Utafiti wa kilimo
unaofanyika ni wa mwaka 2022/23 ambapo tafiti hizi zinaiwezesha nchi kupata Takwimu Rasmi ambazo zitatumika katika kufuatilia na kutathmini
utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya kikanda na Kimataifa.
"Utafiti huu
utafanyika katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara kwa kipindi cha siku 60 na
umeanza Tarehe 5 Novemba 2023. Utafiti huu ni muhimu sana kwa kuwa sekta ya
kilimo inachangia wastani wa asilimia 26.2 ya pato la Taifa, inatoa ajira kwa
karibu asilimia 65 ya watu wote nchini, inatuhakikishia usalama wa chakula na
ina mchango mkubwa kwa maendeleo ya sekta nyingine hususani viwanda.
"Utafiti huu wa
kilimo mwaka 2023/24 utafanyika Tanzania nzima kwenye jumla ya maeneo 1,352.
Kati ya maeneo hayo , 1,234 ni ya Tanzania Bara na maeneo 118 ni Zanzibar.
Jumla ya kaya za Kilimo 16,224 zitahojiwa nchi nzima. Kati ya hizi 14,808 ni za
Tanzania Bara na 1,416 ni za Zanzibar. Utafiti huu utafanyika katika ngazi ya
Kaya na katika ngazi ya Taasisi. Katika Mkoa wetu maeneo yaliyochaguliwa
kufanyika utafiti huu ni 61" Amesema Senyamule
Aidha, Senyamule
ametoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano pindi wanapohitajika kufanya hivyo
kwani kadri wanaposhiriki katika tafiti hizi ndivyo Serikali inapogundua
changamoto mbalimbali zinawakabili na hatimaye kuchukua hatua stahiki. Pia amesema
kushiriki tafiti ni sehemu ya mchango katika kuleta maendeleo ya Mkoa wetu na
maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Tafiti hizi
zinafanyika kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu sura 351 ambayo inaipa mamlaka ya
Kisheria ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kufanya tafiti mbalimbali za Kitakwimu
ili kuzalisha Takwimu kwa ajili ya kutumika katika kutunga na kuhuisha sera,
kupanga mipango na ya maendeleo na kufuatilia na kutathmini
utekelezaji wake.
Kwa Upande wake
Mratibu wa Sensa Mkoa wa Dodoma Idd Muruke amesema tafiti hizo hazikukamilika
kwa wakati ndani ya siku 61 na hiyo ni kutokana na uwepo wa sikuku
zilizopita za mwisho wa mwaka.