Viongozi wa Afrika wampongeza Tshisekedi kwa ushindi
Rais Felix Tshisekedi ataiongoza DRC katika muhula wake wa pili. Picha: AFPVoingozi na wakuu wa nchi mbalimbali wamempongeza rais
Félix Tshisekedi kwa kuchaguliwa tena kuiongoza Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo, kwa mujibu wa matokeo ya Tume Huru ya Uchaguzi DRC, CENI.
Miongoni mwa marais waliompongeza katika ukanda wa Afrika
Mashariki ni pamoja na rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, rais wa Kenya
William Ruto, rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, na rais wa Uganda Yoweri
Museveni.
"Hongera za dhati kwa mheshimiwa Rais Félix
Tshisekedi kwa kuchaguliwa tena Kuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Ninatarajia kuendelea kufanya kazi pamoja katika kukuza uhusiano kati ya nchi
zetu mbili na nchi zetu za Afrika Mashariki," ameandilika rais Samia
katika mtandao wa X, zamani Twitter.
Heartfelt congratulations to
His Excellency, President Félix Tshisekedi on being re-elected as the President
of the Democratic Republic of the Congo. I am looking forward to continuing
working together in fostering the relations between our two countries and our @Jumuiya.
"Rais Tshisekedi amechangia vyema juhudi za eneo hili kwa kuileta Kongo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwa kuturuhusu kufanya kazi na jeshi la Kongo katika kukabiliana na ADF Mashariki mwa Kongo," Museveni aliandika kwenye mtandao wa X.
Nae, rais wa Kenya William Ruto
alimuandikia ujumbe wa kumpongeza kwenye ukurasa wake rasmi wa X.
"Hongera sana ndugu yangu Mheshimiwa Felix
Tshisekedi, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa ushindi uliostahili.
Natarajia kuimarisha uhusiano wa Kenya na DRC kwa manufaa ya nchi zetu,"
ameandika rais Ruto.
Sincere congratulations to my brother His
Excellency Felix Tshisekedi, the President of the Democratic Republic of the
Congo, for a well-deserved victory. The election is a milestone in the
democratic history of your nation. I look forward to strengthening the
Kenya-DRC relations for the mutual benefit of our countries.
Wakati huo huo, rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye
amempongeza Tshisekedi kwa ushindi kwenye uchaguzi huo akimtaja kama
"ndugu na kaka".
Je félicite
vivement mon Homologue et Frère S.E Félix Antoine Tshisekedi pour sa réélection
à la tête de la #RDC suite à la publication des résultats provisoires. En cas d'eventuel
contentieux électoral, je forme le vÅ“u d’une résolution pacifique à travers les
canaux légaux.
Rais huyo wa Burundi Ndayishimiye, ametoa wito kwa upinzani nchini DRC, kutumia njia za kisheria kusaka haki iwapo wanatofautiana na matokeo hayo ya uchaguzi.
Kwa upande wake, rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, alisema Malawi inaungana na watu wa DRC kusheherekea hatua hii ya kidemokrasia kwa mchakato wa uchaguzi wa amani.
Congratulations
to my brother, DRC President Felix Tshisekedi for your electoral triumph and a
new term of office. Malawi joins people of DRC in cherishing this democratic
milestone of a peaceful electoral process. Looking forward to continued ties! #DRCelections
Rais wa Zimbabwe, Mnangagwa, naye aliandika, "Kwa niaba ya serikali, na watu wa Zimbabwe na kwa niaba yangu, ninampongeza sana Mheshimiwa Félix Antonie Tshisekedi Tshilombo kwa kuchaguliwa tena kwa kura kubwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo."
Kulingana na matokeo hayo, Tshisekedi
alifuatwa na mfanyabiashara Moise Katumbi, ambaye alipata asilimia 18 % ya
kura, na Martin Fayulu, ambaye alipokea asilimia 5%. Mshindi wa tuzo ya Amani
ya Nobel Denis Mukwege, naye alipata chini ya 1%.





