UN imeonya kwamba mzozo huo, ikiwa ni pamoja na utegaji wa mabomu kiholela, unahatarisha kuzidisha matatizo ya rasilimali chache za kuhudumia wakimbizi wa ndani zaidi ya 800,000/ Picha : Reuters
......................................................................................
Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya misaada yameonya kuwa mapigano yanayoendelea Mashariki mwa DRC yanahatarisha kuzidisha mzozo wa kibinadamu katika eneo hilo, ambapo zaidi ya watu milioni 5 wamekimbia makazi yao katika majimbo manne.
Matumizi
ya mizinga na makombora makubwa yamesababisha vifo vya watu kadhaa, na
hospitali za Goma zimeshindwa kukabiliana na mmiminiko wa raia waliojeruhiwa.
Mgogoro
unaoendelea kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na waasi wa
M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, umetatiza usambazaji wa chakula katika
mji wa mashariki wa Goma, na kuathiri zaidi ya wakazi milioni mbili na watu
waliokimbia makazi yao.
Esperance
Nyota, mkulima na muuza ndizi, alionya juu ya njaa inayokuja ikiwa mzozo utaendelea
na njia zinazoisambaza Goma kutoka mashamba ya jirani kusalia kukatika.
"Mji
mzima wa Goma unategemea soko hili dogo la usambazaji wa mihogo, mahindi na
ndizi," Nyota alisema.
Takriban
wakimbizi wa ndani 135,000 wamekimbia Sake katika wiki iliyopita, kulingana na
shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi.
Wanaungana
na mamia kwa maelfu ambao tayari wamekimbia makazi yao karibu na Goma tangu
2022 kutokana na mzozo unaoendelea.
Mapigano
yameongezeka tangu kuanza kwa mwaka huu katika miji na vijiji vinavyozunguka
mji mkuu wa mkoa huku waasi wakiteka eneo hilo na kuwalazimu maelfu kutafuta
hifadhi katika mji huo.
Shirika
la Umoja wa Mataifa limeonya kwamba mzozo huo, ikiwa ni pamoja na utegaji wa
mabomu kiholela, unahatarisha kuzidisha matatizo ya rasilimali chache za
kuhudumia wakimbizi wa ndani zaidi ya 800,000, na milioni 2.5 ambao tayari
wamekimbia makazi yao katika jimbo la Kivu Kaskazini.
