NA JOHN BANDA, DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa 79 wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) ambao Tanzania ni mwenyeji.
Mkutano huo utakaoambatana na baadhi ya michezo pamoja na kutembelea baadhi ya vivutio nchini, unatarajiwa kuhudhuriwa na watu 300 kutoka nchi 140 wanachama wa Baraza hilo duniani.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa vyombo vya habari jijini Dodoma Februari 20, 2024, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mkutano huo, Meja Jenerali Francis Mbindi amesema kuwa mkutano huo utakaofanyika jijini Dar es Salaam utaanza Mei 12, 2024 na uzinduzi utanywa na Rais Samia Februari 13, 2024
Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa
sababu kubwa zilizofanya Tanzania iteuliwe miongoni mwa nchi 47 wanachama
wa CISM kutoka Bara la Afrika kuwa mwenyeji wa mkutano huo ni sifa stahiki ilizo nazo kwa mujibu wa kanuni ambazo ni pamoja na uwepo wa huduma stahiki kwa ajili ya mahitaji ya mkutano na
uwepo wa amani,ulinzi na usalama wanchi husika.
Amesema
mkutano huo hapa nchini utafanyika kwa muda wa siku saba kuanzia mei 12 hadi
mei 19, 2024 na unatarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe kutoka nchi zote 140
wanachama wa CISM
“Ni
matarajio yetu kuwa ujio wa wageni hawa nchini kwetu itakuwa ni fursa adhimu ya
kulitangaza Jeshi na Taifa kwa ujumla katika maeneo ya Kijeshi ,Kisiasa,kiuchumi
na kijamii ikiwemo kutangaza na kuendeleza lugha ya Taifa ambayo ni kiswahili
ambayo itakuwa miongoni mwa lugha tano zitakazotumika kwenye mkutano
huo”Amesema
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Michezo ya JWTZ, Kanali Martin Msumari akielezea kuhusu maendeleo ya michezo jeshini. Kushoto ni Meja Jenerali Mbindi.
Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Meja Jenerali, Mbindi kuzungumza na vyombo vya habari.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Zamaradi Kawawa akifafanua jambo.
Baadhi ya maafisa wa JWTZ