Kaimu Mkurugenzi wa Kinga Dkt, Tumaini Nyaonga akizindua Chanjo ya Surua na Rubella kwa kukata utepe katika tukio lililofanyika Leo Februari 16,2024 jijini Dodoma
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. William Mwengee akimuwekea Alama mmoja wa watoto waliochanjwa katika uzinduzi huo
NA JON BANDA, DODOMA
Uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya Chanjo ya Surua na Rubella imezinduliwa Leo Ijumaa Februari 16,2023 Jijini Dodoma huku wazazi na walezi wakitakiwa kuwapeleka watoto wenye umri kuanzia miezi tisa mpaka 59 (chini ya miaka mitano) kupatiwa chanjo hiyo.
Kampeni hiyo ilianza jana Februari 15,2024 katika maeneo mbalimbali nchini na inatarajiwa kukamilika jumapili Februari 18, 2024.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, uliofanyika katika viwanja vya Chinangali Park Jijini hapa,Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kinga Dkt, Tumaini Nyaonga kutoka Wizara ya Afya ambaye alimwakilisha Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema hiyo ni fursa kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao waweze kupatiwa Chanjo hiyo.
"Niwaombe wazazi kuitumia fursa hii kuwapeleka watoto wao waweze kupatiwa chanjo kwani ni muhimu kwa watoto,"amesema Dk Haonga.
Amesema Chanjo hutolewa kila siku ila kampeni hufanyika kila baada ya miaka mitatu au minne.
"Tumepata mrejesho tangu kuanza jana kwa zoezi hili katika maeneo mbalimbali wazazi wamejitokeza kwa wingi,"amesema Dk Haonga.
Amesema zaidi ya watoto milioni 8.9 wanatarajiwa kupatiwa Chanjo katika vituo 7,373 katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha,amewataka Wakuu wa Mikoa,Wilaya na Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia kikamilifu zoezi hilo.
Awali Mwakilishi wa Shirika Afya Duniani (WHO) Dk William Mwengee amesema Tanzania kwa mara ya kwanza ilianza utoaji wa Chanjo ya Surua mwaka 1963.
Amesema jamii inatakiwa kuelimishwa madhara yanayotokana na ugonjwa wa Surua kwani wale wazazina walezi wa zamani wanajua madhara ya ugonjwa huo tofauti na Sasa hivi.
Amesema WHO itaendelea kutoa elimu ikiwemo kwa viongozi wa vijiji kuhusu umuhimu wa chanjo ili kampeni iwe na mafanikio.
Mwisho...