NA JOHN BANDA, DODOMA
BALOZI wa Kuni Poa, Nishati poa Briguettes, Janeth Mtweve toka Kampuni ya Hanny G investment co. LTD amesema kuwa huduma ya ujengaji wa majiko katika taasisi za serikali zikiwemo vyuo na shule za sekondari.
Bi. Janeth ameziweka wazi Pongezi hizo mbele ya Waandishi wa habari Machi 9,2024 Kwenye Kongamano la Nishati Safi na salama lililoandaliwa na Wizara ya Nishati lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma
Amesema Mradi wa Kuni Poa Umesaidia kwani majiko yamekuwa yakipatikana kwa garama nafuu ambayo imewawezesha wananchi kumudu garama zake
Amesema mafanikio ambayo kampuni hiyo imepata ni kutokana na huduma hiyo kupokelewa vizuri ambapo Kwa Sasa wameanza kuwauzia wananchi mmoja mmoja kwa mashriti nafu
" Tunashukuru kwamba Sisi Hanny G tumefanikiwa Sana kujenga majiko mengi katika Vyuo kikiwepo UDOM, na mpaka Sasa wateja wetu wanafurahia huduma zetu, pia tunajivunia Mradi umesaidia kampuni kuongeza uzalishaji wa tani nyingi zaidi, pia kutengeneza majiko kwenye vyuo",
Aidha amesema kuni poa zinazotumika Kwenye majiko hayo kilo 25 zinamaliza mwezi mzima kwa matumizi ya Jikoni kwa familia ya kawaida, ambapo kilo moja inagharimu tsh 600 ikiwa kilo 25 ni TSH 15,000 za kitanzania
Akielezea baadhi ya Faida za kutumia Kuni poa amesema kiuchumi inaokoa garama, inapatina kwa mwaka mzima, hauna moshi wa kumuathiri mtumiaji, huikia miti na kuivisha chakula kwa haraka.




