BANDA MEDIA BLOG

SERIKALI YASEMA BARABARA ZILIZOPO KATIKA HIFADHI ZA TAIFA, TANAPA ZIPO SHWALI

Maafisa kutoka TANAPA wakimsikiliza Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Mobhare Matinyi leo Machi 10,2024 jijini Dodoma wakati akizungumza na vyombo vya habari.

NA JOHN BANDA, DODOMA

KlSERIKALI imesema pamoja na Mvua Ambazo zinazoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo hapa nchini na kusababisha uharibu wa miundombinu  Kwa Sasa  barabara za kwenye hifadhi za Taifa zilizo chini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ikiwemo Serengeti zipo shwali.

 Hayo Yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Mobhare Matinyi  wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dodoma

"Ninautaarifu Umma na wadau wa sekta ya Utalii kwamba TANAPA katika hatua za awali imekamilisha matengenezo na sasa barabara hizo zinapitika na watalii wanaendelea kupata huduma zinazostahili.

Amesema kuwa hakuna Changamoto kubwa iliyotokea kwenye upande wa viwanja vidogo vya ndege Saba vilivyopo ndani ya hifadhi hizo zaidi ya maji kujaaa kwenye baadhi ya maeneo ya kuegesha ndege

Aidha amesema kuwa kwa hatua za Kati TANAPA inataka kunyanyua barabara nzima ya Golini Naabi Seronera yenye kilometa 68 kwa Wastani wa sentimita 50 kutokana na ukaguzi uliofanyika ili kuifanya iwe juu kidogo ya usawa wa ardhi

Ameongeza kuwa barabara hizo pia hupitisha magari ya watalii Kati ya 600 hadi 800 kwa siku hivyo kuharibika mara kwa mara hata kama hakuna Mvua kubwa

"TANAPA inatarajia kwamba utatuzi wa kudumu utapatikana katika barabara kuu zinazoihudumia Serengeti na hivyo kuongeza idadi ya watalii nchini kwa kiasi kikubwa kufuatia matunda ya filamu ya Royal Tour"Amesema

Kuhusu Taarifa za watalii walioingia nchini Kati ya Julai 2023 na Februari 2024 Matinyi amesema kuwa ni watalii 1,451,383





Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG