BANDA MEDIA BLOG

MKUU WA MAJESHI JENERALI JACOB MKUNDA ASHIRIKI IBADA YA PASAKA KANISA KUU LA ANGLIKANA DODOMA

 

 Jenerali Mkunda akifurahia jambo wakati alipokuwa akitoa salamu za Pasaka Kwenye ibada ya sikukuu hiyo iliyofanyika katika kanisa kuu la Anglikana jijini Dodoma 

Askofu Dkt. Cholongani akifafanua Jambo wakati alipokuwa akihubiri kwenye Ibada hiyo.

Mwanasiasa Mkongwe Dkt. John Malecela akizungumza wakati alipotoa Salamu za Pasaka katika Ibada hiyo

Ibada  na maombezi yakiendelea

Sehemu ya Waumini wa kanisa hilo

kwa ya Uvuke ikitoa huduma katika ibada hiyo

Ibada ya Ushirika

  Waumini wakiendelea na Ibada ya pasaka katika kanisa la Anglakana Jijini Dodoma

(PICHA ZOTE NA JOHN BANDA WA BANDA MEDIA ONE. COM)

.........................................................................

NA JOHN BANDA, DODOMA

MKUU wa Majeshi Nchini Jenerali Jacob Mkunda, amesema nchi ipo salama kutokana na uongozi imara wa Serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani.

Jenerali Mkunda ameyasema hayo leo Machi 31,2024 kwenye ibada kuu  ya Pasaka iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ikifanyika Kitaifa katika Kanisa kuu la Aglikana Tanzania, Jijini Dodoma.

“Nataka mtambue kwamba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  inayoongozwa na Mama Dkt, Samia Suluhu Hassan ipo imara, na mimi kama mkuu wa majeshi ya Tanzania niwahakikishie kuwa nchi ipo salama”,amesema

Mkunda ameongeza kuwa Pamoja na usalama wa nchi uliyopo wananchi wahakikishe wanaidumisha amani iliyopo nchini, kwani kuna baadhi ya mataifa ambayo hayawezi kusheherekea sikukuu kama hizi kutokana na kukosekana kwa amani.

“Mwaka huu kuna uchaguzi wa serikali za mitaa na mwaka ujao kuna uchaguzi mkuu, kama hakutakuwa na amani chaguzi hizo hazitaweza kufanyika vizuri, tambueni kuwa amani ni chanzo cha maendeleo ya nchi yoyote hivyo rai, yangu kwa waumini na watanzania wote tuidumishe amani iliyopo”, amesema

Awali akihubiri katika Ibada hiyo Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Dkt. Dickson Chilongani amewataka waumini na wasio waumini wa kanisa hilo kumtanguliza Mungu katika mambo yao Badala ya kumpa masharti.

“Wapo watu wanajitanguliza wenyewe kuliko kumtanguliza Mungu, ukiwasikia hata kwenye maombi yao wakiomba wanampangia Mungu masharti, eti awape Mke wa aina furani au gari aina Furani au kitu chenye hadhi au thamani furani, hiyo ni kujitanguliza mwenyewe tuache ili mapenzi ya yake yatimie”,

Aidha Dkt. Chilongani amesisitiza kuwa Wanawake wathaminiwe na waaminiwe kama Yesu alivyowaamini na kuwathamini.

“Kubwa Zaidi Kumekuwepo Kundi la wanaume ambao wamekuwa wakimzodoa Rais Samia kana kwamba kazi anazozifanya kwa ajili ya Taifa hawazioni kwa sababu tu ni mwanamke, watu wa namna hii ni wabinafsi ambao hawatufai katika jamii yetu”amesema

Amesema katikati ya Mwaka huu kanisa hilo litakuwa na Sinodi ambapo viongozi wa kushika nafasi mbalimbali kanisani watachaguliwa, “niagize kuwe na usawa kusiwe na nafasi maalumu kwa wanaume, wote wagombee kwani wote tupo sawa kama yesu alivyowatumia wanawake kwenda kuwaambia wanafunzi wake kuhusu kufufuka kwake maana wao ndiyo walijitokeza kaburini kabla ya wananume”, amesema

nae Mwanasiasa Mkongwe na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. John Samwel Malecela aliyeshiriki ibada hiyo ya Pasaka wakati akitoa salamu zake amesisitiza Msamaha kwa waumini na wanajamii kwa ujumla kwakuwataka kuondoa visasi na vinyongo mioyoni mwao ili kuruhusu Mungu afanye kazi yake.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG