IKIWA leo ni siku ya Nne ya Maombolezo ya Mzee wa Rukhusa tangu afariki Dunia Mnamo Tarehe 29 Februari 2024 Majira ya Saa 11 jioni, Ambapo mwili wake Ulizikwa Machi 2, mwaka huu Nyumbani kwao Manga Pwani Zanzibar.
Tuendelee Kukipitia Kitabu Cha Safari ya Mzee Mwinyi, ikiwa Jana tuliishia Pale alipoongelea ahueni iliyopatikana baada ya Mashirika ya UMMA kupigwa Mnada na Leo tunaanzia hapa....!!!
Kuhusu tamko la Zanzibar juu ya miiko ya Viongozi anasema lengo lilikuwa zuri kwa kuwa katika uchumi uliokuwa ukikua ilikuwa si sawa kwa Viongozi kuwa malofa. Anasema mazungumzo kuhusu kulegeza masharti ya Miiko ya Uongozi yalikuwa yameanza wakati Mwalimu akiwa Mwenyekiti na alimteua Ngombale aandae mabadiliko mnamo mwezi Oktoba 1990, lakini anasema zigo lilimdondokea yeye wakati wa kikao cha NEC cha Februali 1991 huko Zanzibar kwa kuwa Mwalimu alikuwa tayari amestaafu Uenyekiti wa CCM.
Anasema lengo la Tamko la Zanzibar ilikuwa kwamba Kiongozi awe na uhuru wa kuwa na haki ya kipato binafsi nje ya mshahara nje ya muda wa kazi ya Serikali.
Kuhusu Vyama vingi vya Siasa ameandika kuhusu CCM walivyoridhia, lakini wakaweka tahadhari kuwa pasiwepo na vyama kuungana na pia asiwepo Mgombea Binafsi. Hata hivyo anasema alijitahidi kuendesha vizuri Uchaguzi wa 1995 na kukabiliana na changamoto za Mgombea wa NCCR MAGEUZI Bwana Agustino Lyatonga Mrema na hatimaye CCM ilishinda.
Endelea Kufuatilia BANDA MEDIA ONE.COM uendelee kujifunza Mengi kutoka Katika Kitabu hiki...!!!
