BANDA MEDIA BLOG

WATUMISHI WA SERIKALI TUJISIKIE AIBU TUACHE URASIMU USIO NA SABABU KWA WANANCHI - BITEKO

 

.         


                          .......................................................

JOHN BANDA, DODOMA

NAIBU Waziri Mkuu Dtk. Dotto Biteko  Usiku wa Jumamosi Machi 9,2024 Amezindua Hotel ya Rafiki iliyopo Jijini Dodoma Huku akiwataka watendaji wa Serikali Kuondoa Urasimu katika kuwahudumia Wananchi.

"Nitoe wito Kwa watendaji wa Serikali nikiwemo Mimi Mwenyewe kuwa tuhakikishe tunawahudumia wananchi kwa wakati wanapohitaji huduma

Ifike wakati tujisikie aibu, tuna wajibu wa kulea Sekta Binafsi, mfano Maji, Umeme ,vibari vya ujenzi na idara nyingine Kazi tunayoweza Kuifanya Leo kwanini umwambie mtu aje kesho??  tuache urasimu usio na sababu, yeye ajuaye kutenda mema asiyatende kwake Mtu huyo itakuwa ni dhambi", amesema na kusisitiza

Aidha amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefurahishwa na uwekezaji unaofanywa jijini Dodoma, ambapo ni Makao makuu ya Nchi, na kwamba amejipambanua kwa kuwa mlezi wa sekata binafsi hivyo asingependa kuona wafanyabiashara na wananchi wananyanyasika Kwa namna yoyote.

Kwa Upande wake Mtendaji Mkuu wa Rafiki Hoteli Fladmiry Mallya ameishukuru Serikali kwa Kuweka Mazingira Mazuri ya Uwekezaji yanayomsaidia kila Mtanzania Kuwekeza Nchini kwake

naye Meneja Usambazaji wa Hotel hiyo Fred Zayumba, amesema Hotel hiyo ina Jumla ya vyumba 80 vyenye  ubora Tofauti, kumbi 4 za mikutano, Bwawa la kuogelea, Usafiri kwa wageni, baa na sehemu kubwa  ya maegesho ya magari , ambapo Watanzania 60 wamepata ajira rasmi na 50 zisizo Rasmi, Hotelini hapo. 

Zayumba ameongeza Kuwa ni pamoja na malazi, Chakula na vinywaji vinavyopatikana katika hotel hiyo pia kuna Bwawa la kuogelea, Internet ya bure na Chumba cha Mazoezi.

pia  ameishukuru serikali kwa kushirikiana Bega kwa Bega kwa ukaguzi wa mradi huo wakati wa ujenzi pamoja na kutoa ajira kwa watanzania ambapo wao watahakikisha wanatoa huduma Bora kwa wateja wa ndani na nje ya Nchi.




Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG