NA JOHN BANDA, DODOMA
WAZIRI wa Mipango na
Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo leo A[rili 17,2024 amekutana na waandishi wa Habari jijini Dodoma kwa ajili ya
kuwaeleza kuhusu Nchi ilipotoka ilipo sasa na inapoelekea kwa kutaja mambo
kadhaa ya kujivunia yakiwepo maendeleo hasa wakati huu tunapoelekea kilele cha
maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano
“Tunapopima mafanikio
hatua ya kwanza katika miaka 60 ya muungano ni uhai wa muungano wetu, Kitu cha
pili kuhakikisha kwamba muungano huu unadumu na kulinda amani, utulivu na
mshikamano”, amesema
Aidha amesema Hatua ya
tatu ni kujipima katika maendeleo kwa
kuwa na usalama wa chakula. Wakati ule tumeungana, usalama wa chakula ulikuwa
asilimia 60 huku lengo la nchi ni kujitosheleza kwa chakula kwa asilimia 100 na
kuwa na akiba. Kwa sasa nchi ina usalama wa chakula kwa asilimia 124.
Hatua ya nne ni kujipima
katika maendeleo ni ustawi wa watu na nchi kwa kuangalia mambo ya msingi ya
kibinadamu ikiwemo chakula, mavazi na malazi ambayo nayo tumepiga hatua kubwa.
Wakati tunapata Uhuru,
umri wa kuishi kwa Mtanzania ilikuwa wastani wa miaka 32, mwaka 2000 umri wa
kuishi ukasogea hadi wastani wa miaka 52. “Tamaa yetu ifikapo mwaka kesho 2025
wastani wa kuishi uwe miaka 68. Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, ilionyesha
wastani wa kuishi ni miaka 66”, amesema
Mambo matatu ya kufanya
kukuza ustawi wa binadamu ni kumpa binadamu elimu ili aweze kuishi vizuri
ambapo mwaka 2000 nchini Tanzania, kiwango cha kuandikisha wanafunzi kilikuwa
asilimia 69. Kwa malengo tuliyojiwekea kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa ya
mwaka 2025, ni kufikia asilimia 100 ya uandikishaji wa wanafunzi ambapo hadi
sasa tumevuka malengo, tupo asilimia 108.5.
Kuhusu suala la kwenda
sekondari, mnamo mwaka 1964 ilikuwa asilimia 5, mnamo mwaka 2000, watoto
waliofanikiwa kufika sekondari kutoka shule za msingi ilikuwa chini ya asilimia
20. Lengo letu ifikapo mwaka 2025, tuwe tumefika asilimia 48. Kwa takwimu za
hivi sasa, tupo asilimia 70.
Dira ya Maendeleo ya Taifa
inayokuja, tutahitaji elimu ya msingi Tanzania iwe kwa Watanzania wote na wote
lazima kufika sekondari kwa asilimia 100.
Eneo lingine katika kukuza
ustawi wa binadamu ni afya hasa kwenye eneo la mama na mtoto, na la tatu ni
maji ambapo wakati tunapata uhuru, uwepo wa maji vijijini ulikuwa chini ya
asilimia 15 na mwaka 2000 ilikuwa asilimia 32. Kwa sasa ni asilimia 77.
Nchi inahitaji uwepo wa
uchumi, kukua kwa uchumi ni nyenzo muhimu. Ili nchi ione inapiga hatua ni
lazima iangalie uchumi unaendaje.
Tanganyika na Zanzibar
ziliungana Aprili 26, 1964 ambapo kila mwaka maadhimisho ya Muungano huo hufanyika
kila tarehe na mwezi huo kama ilivyo kwa mwaka huu ambao kilele chake kitafanyikia
Uwanja wa Uhuru jijin Dar eslaam.

.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)