BANDA MEDIA BLOG

KATIBA YA TANZANIA: Rais Ana SIKU 14 Kuteua Makamu wa Rais Mpya

Katiba ya Tanzania: Rais Ana SIKU 14 Kuteua Makamu wa Rais Mpya
Rais Ana SIKU 14 Kuteua Makamu wa Rais Mpya

Wakili wa Mahakama Kuu, Ferdinand Makore amesema kwa mujibu wa Katiba baada ya Makamu wa Rais kujiuluzu, Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan atamteua Mtu mwingine mwenye sifa ndani ya siku 14 tangu kujiuzulu kwa Makamu wa Rais kisha jina hilo litapaswa kuthibitishwa na Bunge la Tanzania ili aapishwe kuwa Makamu wa Rais wa Nchi.

Akizungumza na Ayo TV, leo 25,2026 Makore amesema “baada ya kiti cha Makamu wa Rais ndani ya siku 14 Rais atateua Mtu na Mtu huyo itabidi athibitishwe na Bunge, kwahiyo muda ambao tunao ni siku 14 tangu kujiuzulu kwa Makamu wa Rais, kwahiyo kama Nchimbi amejiuzulu kwa mujibu wa Ibara ya 149 ibara ndogo ya pili basi siku 14 zitahesabiwa kuanzia Septemba 04,2026 hilo ndio jukumu la Rais kutafuta Mtu wa kuziba nafasi ambaye atathibitishwa na Bunge”

“Mtu huyo ambaye atapelekwa Bungeni kuthibitishwa anatakiwa awe na sifa za Kiongozi anayefaa kuwa Makamu wa Rais ambazo zinaainishwa kwenye ibara ya 47 ibara ndogo ya nne, ambapo anatakiwa kuwa Raia wa Tanzania, atimize umri wa miaka 40 na kuendelea, awe Mwanachama wa Chama cha Siasa ambacho Mgombea Urais anatumikia, na anayeweza kuwa na sifa za kugombea ubunge, katika kipindi cha miaka mitano kabla ya kuteuliwa anatakiwa asiwe ameshtakiwa au kutiwa hatiani katika makosa ya ukwepaji wa kodi au kudaiwa na Serikali”

“Rais anaweza kumteua Mbunge kushika madaraka ya Makamu wa Rais kama kiti cha Makamu wa Rais kipo wazi kisha Mbunge huyo atathibitishwa na Wabunge wenzake na Jimbo lake litakuwa wazi kwa ajili ya uchaguzi mdogo kufanyika”

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG