Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kinga,Wizara ya Afya,Dk.Tumaini Haonga akizungumza jambo
Waandishi wa habari wakiwafuatilia matukio kwenye warsha hiyo
Waandish wa Habari jijini Dodoma wakifuatilia jambo wakati walipokuwa kwenye Warsha ya Saratani ya Mrango wa Shingo ya Kizazi iliyotolewa na Wizara ya Afya Kitengo cha Chanjo
..............................................................
NA JOHN BANDA, DODOMA
AFISA mipango wa Chanjo Taifa
(MOH) Lotalis Gadau amesema Takwimu zinaonesha kunakuwa na maambukizi
mapya ya ugonjwa wa saratani ya Mlango wa Kizazi kwa wanawake zaidi ya Milioni
10, huku wanaopoteza maisha ni zaidi ya Milioni 6 Barani Afrika kwa kipindi
hicho.
Afisa Mpango kutoka Wizara
ya Afya akitoa mafunzo kwa waandishi wa Habari, kuhusu chanjo ya saratani ya
mlango wa shingo ya kizazi (HPV) kuelekea maadhimisho ya Wiki ya chanjo ambayo
itaanza Aprili 22 hadi 28 mwaka huu amesema Zaidi ya Watoto wenye umri kuanzia
miaka 9 hadi 14 atapatiwa chanjo hiyo.
Kutokana na hilo Gadau
amebainisha kuwa Tanzania ni nchi ya Tatu kwa kuwa na idadi kubwa ya Wagonjwa
wa Saratani ya Mlango wa kizazi katika Bara la Afrika ikitanguliwa na Nchi Jirani
ya Uganda
Pamoja na hayo amesema
kuwa wagonjwa wengi takribani 70% wamekuwa wakifika katika Vituo vya Afya
wakiwa na hali mbaya na kutoa wito kwa jamii kuhakikisha wanakuwa na utaratibu
wakupima Mara kwa mara ili kuwa rahisi kupata matibabu iwapo kutakuwa na
kubainika maambukizi.
Akielezea kuhusu Chanjo ya
Saratani ya Mlango wa shingo ya kizazi amesema Chanjo hiyo ni salama na ni dozi
ya Mara moja na inatolewa tofauti na awali ilikuwa inatolewa kwa awamu mbili ambapo
wanaopatiwa chanjo hiyo ni watoto wakike kuanzia umri wa miaka 9 hadi 14.
Ni muhimu sasa kwa wazazi
kuhakikisha wanawahamasiha Watoto wao kujitokeza kupata Chanjo hiyo ya HPV ili
kuwalinda na maambukizi ya ugonjwa huo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi
Idara ya Kinga,Wizara ya Afya,Dk.Tumaini Haonga amesema kutokana na ugonjwa
kuwa na Kinga Serikali imeamua kuwe na Mpango wa kutoa Chanjo hiyo kwa Watoto
na mabinti ili kupambana na ugonjwa huo.
Dkt. Haonga amesema baada ya utafiti na ufuatiliaji wa mara kwa mara unaofanywa na shirika la Afya Duniani (WHO) Pamoja na wadau wengine Imeinika chanjo ya Pili imekuwa ikiachwa kutokana na hapo awali kuwa wanapewa Watoto wenye umri wa miaka 14 ambao pia walikuwa wakimaliza darasa la 7.