NA JOHN BANDA, DODOMA
JUNE 13, siku ya Alhamis Mawaziri wa Fedha wa Nchi za
Africa Mashariki Wamesoma Bajeti Kuu za Serikali zao kwa mwaka huu wa Fedha wa
2024/25 ambazo zinaingia kujadiliwa na Mabunge ya Nchizo ambapo kwa Tanzania
Jumuiya ya wazazi ya Chama kinachoongoza Dola cha CCM kimetoa pongezi kwa
makadilio hayo ya Bajeti yaliyosomwa na Waziri mwenye Dhamana hiyo Dk. Mwigulu
Nchemba
Pongezi hizo zimetolewa mapema leo June 14,2024 na
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Fadhari Rajabu Maganya
wakati akiongea na Waandishi wa Vyombo mbalimbali vya Habari jijini Dodoma.
Amesema kuwa
bajeti imejaa matazamio mema ambayo yanabeba maisha ya wananchi wa Tanzania kwa
kuboresha huduma mbalimbali Kama ambazo zilitajwa na Mhe.Waziri Nchemba.
"Sisi Jumuiya ya Wazazi Mimi kama kiongozi wake
ninampa Mhe.Rais Kongole,Kongole hii ni kwa kuwa bajeti hii inabeba matumaini ya
Watanzania, kwa hiyo tukaona kama Jumuiya tutoe kauli yetu ya kuipongeza
Serikali kwa namna ambavyo imeendelea kuwajali watanzania na kuwapatia nafuu ya
maisha kadri inavyowezekana"amesema
Aidha amesema kuwa Tanzania si nchi
iliyoendelea,Tanzania ni nchi inayoendelea kwa hiyo Maendeleo ni mchakato.
"Kwa hiyo tunaungana na Mhe.Rais na Serikali
yake ya Chama Cha Mapinduzi ambayo anaiongoza kwa namna ambavyo anaguswa na
maisha ya wananchi na kwa kweli sote ni mashahidi tunaona anavyojitahidi kuupiga
mwingi kwa kushuhulikia miundombinu na kero mbalimbali za wananchi” amesema
Aidha amesema kero ya kikokotoo imekuwa ikiimbwa sana
kwa siku za hivi karibuni lakini Serikali imeliona hilo na kulipatia majibu kwa
vitendo kwa kuongeza toka asilima 33 iliyokuwapo awali mpaka kufikia asilimia
40,
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amempongeza
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi
kwa bajeti ambayo imegusa maisha ya Wazanzibar na Watanzania kwa ujumala.
Hapo jana Juni 13,2024 Waziri wa Fedha
Mhe.Dkt.Mwigulu Nchemba aliwasilisha Bungeni mapendekezo ya bajeti ya jumla ya
Shilingi trilion 49.345.7 kwa mwaka 2024/2025,ambapo ni sawa na ongezeko la
asilimia 11.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/2024 ya shilingi trilion
44.388.1