BANDA MEDIA BLOG

Nani anaetunza funguo za Al-Kaaba mahali patakatifu kwa Waislamu?

sd

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Aya za Quran zimeandikwa kwenye ufunguo na kufuli.

Dokta Saleh bin Zainul Abedin Al Shebi, mtunzaji wa funguo za Kaaba ama Al-Kaaba, eneo takatifu zaidi kwa Waislamu, amefariki dunia.

Inaaminika familia yake ilipata ufunguo huu wakati wa Mtume Mohammad na imekuwa na ufunguo huo tangu wakati huo.

Kwa karne nyingi, familia ya Dk. Sahel bin Zainul Abedin imebeba jukumu la kuuweka ufunguo huo salama. Dk. Saleh alikuwa mrithi wa 109 wa familia ya Al Shebi, aliyepewa jukumu la kutunza ufunguo huo.

Ufunguo ulikabidhiwa kwa Dk. Saleh baada ya kifo cha mjomba wake Abdul Qadir Taha Al Shebi 2013.

Dk. Saleh, aliyesoma PhD yake ya Masomo ya Kiislamu kutoka Chuo Kikuu cha Umm Ul Qura, alizaliwa katika jiji la Makka mwaka 1947. Mekka inachukuliwa kuwa jiji takatifu zaidi katika Uislamu.

Alifundisha akiwa mhadhiri katika chuo kikuu hicho kwa miaka mingi. Pia alichapisha makala nyingi za utafiti na vitabu vinavyohusiana na Uislamu.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG