Hamasa zimeendelea kujitokeza mtandaoni huku kizazi
cha Gen Z kinachoongoza maandamano dhidi ya serikali nchini Kenya kikichapisha
orodha ya matakwa 10 wanayoitisha kutimizwa na serikali.
Vijana hao walianza maandamano yao kupinga mswada wa
fedha 2024 kuanzia Juni 18 lakini licha ya Rais William Ruto kuridhia na
kutangaza kuondoa mswada huo, bado vijana hao wamesisitiza kuendelea na
maandamano huku wakimtaka Rais kujiuzulu.
Licha ya yote, vijana hao wanasema hawana kiongozi
wala uhusiano wowote na chama cha kisiasa au kabila, na kuwa wanapigania haki
ya vizazi vichanga na vijavyo.
Msimamo mkali
Orodha, imetokeza mtandaoni (ambayo haijathibitishwa
chanzo chake) ikionyesha matakwa 10 wanayodai lazima yatimizwe na Rais Ruto
kabla ya kutuliza hasira zao.
Pia wametaka serikali
ichapishe maelezo ya namna fedha zote za serikali zilitumika katika kipindi cha
mwaka 2023.
Miongoni mwa mambo makuu yanayodaiwa ni Kutii maagizo
yote ya mahakama, kufuta ufadhili wa ofisi ya mke wa rais na mke wa naibu rais
na kupunguzwa mishahara ya wabunge kutozidi shilingi 200 000 za Kenya.
Vijana hao wamadai kuwa fedha hizo badala yake
zitumike kulipa mishahara ya walimu na madaktari.
Orodha hiyo ambayo imechapishwa na watu wengi
wakiwemo baadhi ya wanasiasa katika mtandao wa X pia imeitisha kuondolewa
ushuru wa nyumba na kurejeshwa fedha zilizotozwa kwa wafanyakazi kuelekea hilo.
Pia wametaka serikali ichapishe maelezo ya namna
fedha zote za serikali zilitumika katika kipindi cha mwaka 2023.
Japo hakuna thibitisho orodha hiyo imetolewa na nani
au uhakiki wake, imeendelea kusambazwa mtandaoni.
Taarifa kutoka kurugenzi ya mawasiliano ya Rais
ambayo pia ilichapishwa mtandaoni ilikuwa imeelezea awali kuwa serikali inataka
kufanya mazungumzo na vijana kuangazia masaibu yote walioyotaja na kutafuta
suluhu ya kudumu.

