Wanamgambo wa kikundi cha M23 wameendelea kushika
hatamu katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku miji
mingi zaidi ikiangukia mikononi mwa waasi hao, chanzo kimoja kimeliambia
shirika la habari la AFP siku ya Jumapili.
Kinshasa inaituhumu Rwanda kwa kukiunga mkono kikundi
cha Kitutsi cha M23 ambacho kinashikilia maeneo mengi ya mashariki ya DRC,
tuhuma zilizopingwa na Kigali.
Siku ya Jumapili, kikundi cha M23 kiliingia kwenye
mji wa Kirumba, kaskazini mwa Kivu, eneo lililotawaliwa na vurugu toka mwaka
2021.
Kirumba ni mji mkubwa kusini mwa eneo la kibiashara
la Lubero lenye wakazi zaidi ya 120,000.
Kuelekea kaskazini
"Tunasikitika kuona kuwa toka jana, sehemu kubwa
ya mji uko mikononi mwa M23," alisema ofisa mmoja ambaye hakutaka jina
lake litajwe, aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumapili.
Kulingana na ofisa huyo, kikundi hicho kilikuwa
kinaelekea kaskazini mwa mji huo.
Siku ya Jumamosi, kikundi cha M23 kilishikilia mji wa
kimkakati wa Kanyabayonga, huku maeneo mengine yakiwa chini ya udhibiti ya
waasi hao.
Kanyabayonga ni eneo lenye wakazi zaidi ya 60,000
huku wengine wengi wakiwa wamekimbia eneo hilo kutokana na uwepo wa waasi hao.
Rais aitisha kikao cha dharura
Mji huo unachukuliwa kuwa njia ya kuelekea Butembo na
Beni kaskazini, ngome za kabila la Nande na vituo vikuu vya kibiashara.
Ipo katika eneo la Lubero, mji wa nne kaskazini mwa
Kivu ambalo waasi hao walitumia kuingilia baada ya Rutshuru, Nyiragongo na
Masisi
Siku ya Jumamosi, Rais Felix Tshisekedi aliitisha
baraza la ulinzi la taifa.
Wakati wa hotuba ya kuadhimisha siku ya uhuru wa nchi
hiyo, Tshisekedi alisema "maelekezo ya wazi na madhubuti yametolewa kwa
ajili ya kulinda uadilifu wa eneo la nchi yetu", pasipo kutoa maelezo
zaidi.
Uhamisho mkubwa
Miji mingine karibu na Kanyabayonga pia yapo chini ya
udhibiti wa M23, kulingana na vyanzo vya kiusalama.
Eneo la DRC lenye utajiri wa madini limeshuhudia
vurugu za miaka 30 kutoka vikundi vyenye silaha.
Katika ripoti yake ya kila mwezi siku ya Ijumaa,
ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, eneo hilo limeshuhudia uhamaji
mkubwa wa watu.
