........................
NA JON BANDA, DODOMA
TUME ya vyuo vikuu (TCU) imekutana jijini Dodoma kwa
ajili ya kufanya mapitio na marejeo ya Mitaala Mipya Huku Mgeni Rasmi akiwa
Profesa Adolf Mkenda Waziri katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
ambaye ameweka Msimamo wa Serikali kuwa Walimu Wapya watafanya Mitihani kabla
ya Kuajiliwa.
Mkenda ameitoa Kauli Hiyo June 7,2024 kwa waandishi
wa Habari mara baada ya kumaliza kutoa hotuba ambayo alisema si ya kufungua
wala kufunga mkutano huo uliowakutanisha, Makamu Wakuu wa Vyuo Vikuu na
Vyuo vya Kati, Wakuu wa Vyuo Vikuu vishiriki Manaibu Makamu Wakuu wa Vikuu
upande wa taaluma na wadau wa mbalimbali wa elimu .
Profesa Mkenda amesisitiza kuwa katika kutekeleza
mitaala mipya ya elimu, walimu wapya watafanya mtihani kabla ya kuajiriwa na
kwamba watakaofanya vizuri ndio watakaopata nafasi.
Prof Mkenda amesema ni muhinu wanaojiriwa kwa sasa
kama walimu watafanya mtihani kama Kada zingine wanavyofanya lengo likiwa ni
kupata walimu bora Zaidi.
"Tukumbuke kauli ya Mheshimiwa Rais (Samia
Suluhu Hassan) tukiwa Zanzibar alisema jamani tumefika mahali tuna walimu
akitafuta kazi anasema mimi nimekosa kazi ila anaambiwa hata ualimu
umekosa? Sasa hivi tunaenda sehemu ambayo mwalimu unakuwa bora na kazi yetu
kubwa sio kuangalia watu wangapi wameajiriwa kazi yetu ni watu wangu wamepata
walimu gani bora wa kufundisha,"amesema Prof Mkenda.
Kuhusu walimu kuwa na leseni amesema : "Kwa Sasa
naomba nisilizungumze hili utaratibu utakapokamilika litatangazwa,"
Aidha, amesema kwa mujibu wa sera ya elimu
wataendelea kuwaendeleza walimu waliopo makazini kwa kutumia rasilimali
zilizopo.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu
(TCU) Profesa Charles Kihampa amesema lengo la kikao hicho ni kujadiliana
kwa pamoja kuhusiana na utekelezaji wa mabadiliko ya mitaala ya elimu.
Amesema wanataka ifikapo mwaka 2025-2026 mitaala yote
iwe imefanyiwa mabadiliko kwa kuzingatia maoni ya wadau.
"Kuna haja ya kijipanga mapema ndio maana tumekutana hapa ili tuweze kujadiliana kwa mapana na kutoka na majibu sahihi kuhusiana na mitaala yetu,"amesema Prof Kihampa.