NA MWANDISHI WETU, DODOMA
UMOJA WETU NDIYO NGUVU YETU ………. !!!!!!
WANAWAKE Wilayani Chamwino wametakiwa kuacha kubweteka majumbani wakisubiri huduma kutoka kwa wenza wao pekee kwani kuna wakati hata wao hufikia wakati wanakwama.
Pia wametakiwa kutowacha wenzao majumbani wakiwa hawana cha kufanya badala yake wakawaibue na kama kuna vitendo vya ukatili ambavyo wanawake wenzao wamekuwa wakifanyiwa wakaviibue.
Hayo yamesemwa Juni 29,2024 Kwenye kikao cha wanaumoja wa amani kwanza katika kata ya Mpwayungu wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma, na Makamu Mwenyekiti wa Idara ya wanawake wa Taasisi ya Umoja wa Amani Kwanza Judith Jenaro akiwa kwenye ziara ya kikazi
Bi. Judith amesema wanawake wakijishughulisha watawasaidia wenza wao katika malezi ya familia badala ya kubweteka majumbani wakisubiri kuletewa.
“wanawake tujitahidi kushughulisha na shughuli za kujiingizia kipato hata kama ni kidogo bila kuwaachia wanaume peke yao kwani hata wao kuna wakati hujikuta mambo hayaendi sawa”, amesema
Aidha amesema ifike hatua wanawake wakashikamane wakawe kitu kimoja kwa kushirikiana kwani kwa kufanya hivyo watawasaidia hata wale wananwake ambao wamekuwa wakikumbana na vitendo vya ukatili toka kwa waume zao.
“tukishirikiana tuhakikishe tunashikana mikono wenyewe kwa wenyewe kwa upendo ambapo kwa njia hiyo tunaweza kugundua vitendo vya ukatili ambavyo baadhe ya wanawake wenzetu wamekuwa wakifanyiwa lakini pia hushindwa kuvisema kutokana na vitisho wanavyokumbana navyo toka kwa wenzi wao”, amesema
Mkuu Wa Idara ya Habari UAK, Taifa John Banda ametumia nafasi hiyo kuwajulisha wakazi hao wa Kata ya Mpwayungu Wilayani Chamwino Mkoa Wa Dodoma kuwa ni Muhimu kutunza amani kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa maana uwepo wa Amani husababisha kila kitu kiweze kufanyika bila shida ikiwemo kupiga vita umasikini.
“uwepo wa amani husababisha ndoa kudumu, mipango ya kupiga vita umasikini kufanikiwa, familia kutogawanyika, ibada na shughuli nyingine za maendeleo kufanikiwa bila kizuizi tofaut nan chi nyingine ambazo hufanya ibada huku Bunduki zikiwa Mkononi”, amesema
Aidha amesema amani ni dawa ya Chuki na Magomvi yasiyo na Sababu, mtu mwenye amani anakuwa na kinga ya Stress hata magonjwa yanayosababishwa na Sononeko la Moyo Humuepuka, hivyo kila mtu aitunze na kuilinda amani ya nchi iliyopo Pamoja na kuiishi.
Pomoja na Makamu Mwenyekiti wa Idara ya Wanawake UAK, Taifa, Mkuu wa Idara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo John Banda pia katika ziara hiyo waliongozana na Katibu Msaidizi wa UAK. Mkoa Wa Dodoma Dkt. Chuma Pamoja na Wema Adamu Juma.
Ziara hiyo ya Idara ya Wanawake iliyoanzia Wialayani Chamwino itakwenda Mkoa mzima katika wilaya zote 7 za Mpwapwa, Kongwa, Chemba, Bahi, Kondoa na Dodoma Mjini.
‘TUKUTANE DODOMA KWENYE JAMBO LETU, JULAI 23,2024”,
IMETOLEWA NA JOHN BANDA, MKUU WA IDARA YA HABARI, SANAA, UTAMADUNI NA MICHEZO UAK, TAIFA