Akisoma Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, Bungeni-Dodoma, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kufikia Mei 2024, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini imeunganisha Umeme katika Vijiji 11,973 sawa na 97.2% ya Vijiji vyote Nchini
Ameongeza kuwa Vitongoji 32,827 Nchi zima vimefikishiwa Umeme, na kazi inaendelea hadi Vitongoji vikamilike
Pia, hadi kufikia Desemba 2023 hali ya upatikanaji wa Huduma ya Maji safi Vijijini ilifikia 79.6% na 90% katika maeneo ya Mijini ambapo Mafanikio hayo yamechangiwa na kukamilika kwa Miradi 1,633 ya Maji Vijijini pamoja na 213 kwa Mijini.
