BANDA MEDIA BLOG

JAMII IELIMISHWE UMUHIMU WA KUTUNZA NA KUHESHIMU UTU WA BINADAMU; M/KITI WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU

 


                             ............

               NA JOHN BANDA, DODOMA

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Nchini,imewashauri Viongozi wa Siasa  na  Dini,kuielimisha Jamii juu ya umuhimu wakutunza na kuheshimu  utu wa  binadamu.

Pia Tume hiyo imeisisitiza  Serikali kuongeza idadi ya Askari na bajeti ili kukabiliana na mauaji yanayotokea pamoja na kulitaka Jeshi la Polisi kuongeza jitihada za kuzuia makosa yasitokee.

 Akiongea Ofisini kwake, Jijini Dodoma mbele ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari, Mwenyekiti wa Tume hiyo,Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu, amesema viongozi hao wakatoa elimu hiyo itakayosaidia kuondoa matukio ya mauaji ambayo yamekuwa yakitokea katika maeneo mbalimbali ya nchi.

 Jaji Mwaimu  ametoa mfano wa mauaji ya Mtoto mwenye  Ualbino, Asimwe Novart ambaye alichukuliwa nyumbani kwao Kamachumu Mkoani Kagera May 30, 2024 na baadae mwili wake kukutwa kwenye kalavati, June 17,2024 akiwa ameuawa na kukatwa baadhi ya viungo vya mwili wake.

 “viongozi wa kisiasa na dini mnaona vitendo vinayofanywa juu ya watu wenye ulemavu wa Ngozi, kutokana na Imani za kishirikina ambazo husababisha watu wasio na hatia kuuliwa kwa lengo la kutaka kutajirika kupitia viungo vya watu hawa

 watoe elimu ili jamii ijue umuhimu wa kutunza na kuheshimu  utu wa  binadamu wenzao”, amesema

ameongeza kuwa  Serikali ione umuhimu wa kuweka nguvu katika maeneo ya mipakani hasa mikoa ya kaskazini Magharibi ambako matukio kama hayo yamekuwa yakijitokeza kwa madai hayo ya Imani za kishirikina “ati viungo vya albino vinaweza kusababisha upatikanaji wa madini kwenye migodi na pia uongozi kwa wagombea wa kisiasa

 Napenda kutoa wito kwa Serikali yetu kuhakikisha inaliongezea nguvu Jeshi la Polisi kwakuongeza idadi ya Askari ili waweze kukidhi mahitaji Pamoja na kuongeza bajeti ya vifaa ambavyo ni vitendea kazi ili waweze kufika kwa haraka pale matuko ya kihalifu yanapotokea”, amesema

 Licha ya ,hayo Mwaimu amebainisha kuwaTume ya Haki za Binadamu na utawala bora,imekuwa ikipokea  malalamiko mengi   kuhusu migogoro ya Ardhi Nchini, ambapo Mkoa wa Dodoma ndio unaongoza na  changamoto kubwa  ikiwa  kutokuwepo kwa ushirikishwaji.

“Suala la mipango miji ni zuri katika uendelezaji wa miji hasa pale watu wa ardhi wanapokuwa wanafanya upimai ni vyema wakakaa na wananchi na kuwashirikisha ili kuondokana na migogoro hiyo”.

 Katika hatua nyingine,amesema  wamekuwa wakipokea malalamiko ya watumishi wa Umma kulalamikia ucheleweshwaji wa mafao kwa wastaafu,mapunjo ya mshahara pamoja na Kikokotoo.

 Hivi karibuni matukio kadhaa ya mauaji yameripotiwa likiwemo  la wilayani chamwimo  julai 7, 2024 majira ya saa 4:30 asubuhi huko kijiji cha mheme, mtoto  Goodluck mathias mwenye umri wa miaka 5 alinyongwa na baba yake wa kambo, Steven Mabula mwenye umri wa miaka 44 ambapo chanzo cha tukio hilo, Steven alirudi nyumbani na mke wake wakiwa wamelewa wakaanza kugombana kisha mkewe kukimbilia kwa jirani kujificha na aliporudi akakuta mtoto wake ameshanyongwa na baba huyo wa kufikia.

 Siku chache Baadae Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma,  Theopista Mallya alibainisha mbele ya waandishi wa Habari kuwa ndani ya Wiki mbili tayari watu 5 walishauawa kutokana na visa vinavyosababishwa na ulevi.

MWISHO 

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG