BANDA MEDIA BLOG

KAMPUNI ZA MABASI ZA SHABIBY LINE NA SATCO ZAKIMBIZANA KWA KUTOA HUDUMA BORA ZA USAFIRISHAJI NCHINI

 

NA JOHN BANDA, DODOMA

KAMPUNI za Mabasi za SHABIBY LINE na SATCO zinazotoa huduma za kusafirisha Abiria kwa njia ya Barabara zimekabidhiwa Tuzo ya mshindi wa kwanza na ya pili baada ya kuibuka washindi  katika utoaji wa Huduma hiyo kwa abiria hapa nchini.

Tukio la kukabidhiwa tuzo hizo limefanyika Agosti 26,2024 katika uwanja wa jamhuri jijini Dodoma, kwenye Uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Kitaifa na Maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambapo Makamu wa Rais. Dkt. Philip Mpango amekuwa Mgeni Rasmi.

Akiongea kwa Furaha baada ya Kupata Tuzo hiyo Brand Manager wa Kampuni ya SHABIBY LINE Nicolaus Johachim amesema Siri iliyowafanya kuibuka washindi, ni Kutoa huduma kwa kuzingatia viwango vya Ubora Pamoja na kuziishi sheria za barabarani kwa ajili ya Usalama wa Abiria na wafanyakazi.

“kwa upande wetu shabiby line tuzo hii Pamoja na zingine tulizowahi kuzipata huwa tunazielekeza kwa Abiria na wateja wanaotumia huduma zetu, na kwamba tunawaahidi kuendelea kutoa huduma bora zenye viwango vya kitaifa na kimataifa ambazo zitaendelea kwavutia wateja wetu:, amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabasi ya SATCO iliyoibuka mshindi wa Pili, Rubaiye Mabighut amewashukuru wateja wao kwa kuwawezesha kupata tuzo hiyo lakini pia LATRA ambao wametambua mchango wao katika utoaji wa huduma ya usafirishaji katika jamii ya Watanzania kiasi cha kuwapa Tuzo ya mshindi wa pili.

“hatuna mengi ya kuwaahidi wateja wetu kwani huduma bora ni sifa yetu kubwa, ndiyo maana kwa kuzingatia usalama wa abiria tunazingatia sheria za barabarani hivyo Mabasi ya Kampuni yetu ya SATCO kutokua katika kundi la Ajali za Barabarani”, amesema na kuongeza 

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG