BANDA MEDIA BLOG

MKURUGENZI MKUU TASAF ATEMBELEA BANDA LAKE NANE-NANE DODOMA, AKUTANA NA WANUFAIKA

 
Mkurugenzi mkuu wa Tasaf Shedrack Mziray akimuelekeza jambo mmoja wa wanufaka wa Mpango huo wa kunusuru kaya masikini ambaye kwa sasa amebadilisha maisha kwa kufanya kazi za mikono.

NA JOHN BANDA, NANE-NANE DODOMA

Mkurugenzi mtendaji wa Mpango wa Kunusuru kaya Masikini (TASAF), Nchini Shedrack Mziray  leo Agosti 7,2024 ametembelea banda lake la maonyesho lililopo katika viwanja vya Nane nane Nzuguni jijini Dodoma na kujionea kazi mbalimbali za mikono zinazofanywa na wanaufaika wa mpango huo.

Akiongea Baada ya kujionea kazi hizo amewapongeza wanufaika hao ambao wanatengeneza Mikoba ya wanawake, batiki, vyakula vya usindikaji, sabuni, vyungu na mapambo ya aina mbalimbali ikiwemo kilimo kutokana na ruzuku wanazozipata toka serikalini.

Mziray amesema serikali inaangalia uwezekano wa kuungana na taasisi nyingine ikiwemo SIDO ili wanaufaika hao waweze kupewa elimu ya ufundi wa kazi zao ili waweze kutengeneza bidhaa bora zaidi ambazo zikiingia sokoni ziweze kufanya vizuri ikiwemo kuwapa manufaa walengwa.

amesema kwa sasa TASAF inahudumia kaya Masikini 1.3 mil kutokana na takwimu zilizotolewa na NBS kwamba asilimia 8 ya watanzania ndizo zilizo katika hali mbaya zaidi.

 






Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG