NA JOHN ISAREAL, NANE-NANE DODOMA
KAMPUNI ya Swissport pl Tanzania inayotoa huduma za Kupokea, Kuhifadhi na kusafirisha
Mizigo nje ya nchi imewahamasisha wakulima na wote wenye nia ya kusafirisha
mizigo nje ya nchi kufanya hivyo kwani Garama ni nafuu tofauti na uelewa wa watu
wengi.
Mratibu wa Shughuli
za Usafirishaji Mizigo Nje ya Nchi,
Denis Ngaila amemwambia Mwandishi wa Habari hizi, kwenye Maonyesho ya Kilimo na
Mifugo yanayofanyika katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni jijini Dodoma kuwa
wapo watu wanaodhani masharti ni magumu au garama ni kubwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Metl, Indrabhuwan Singh akifafanua jambo wakaati alipokuwa akiongea na Organstus Hatiro,Denis Ngaila ambao ni Waratibu wa Usafirishaji wa Mizigo wa Kampuni ya SWISSPORT, katika viwanja vya nanenane jijini Dodoma leo Agosti 8,2024
Ngaila amesema Kampuni
hiyo inasafirisha Matunda, Nyama, Maua na hata mizigo mingine kuwa watu wenye
nia ya kutaka kuhudumiwa wafike katika viwanja hivyo vya nanane lakini pia
kwenye ofisi zao zilizopo kwenye viwanja vya ndege vya Mwalimu Julius Nyerere
na Kilimanajoro KIA.
Hata hivyo Mratibu
huyo amesema wametoa na wanaendelea kutoa Elimu ya kutosha katika maonyesho
hayo na kwamba mwitikio ni Mkubwa kwa wakulima hasa wa Parachichi. ambao
wamekuwa wakisafirisha zao hilo kwa wingi kwenda nchi za bara Ulaya, Asia na
kwa africa ni Afrika Kusini na Kenya.