BANDA MEDIA BLOG

NJOONI NANE - NANE DODOMA MMUONE NG'OMBE DUME UZITO KG 950 ALIYEZAA NDAMA 206, AKIWA NA UMRI MDOGO/ SINGITA



/NA JOHN ISAREAL, NANE-NANE DODOMA

KWENYE Maonyesho ya Kilimo na Mifugo yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nane nane Kitaifa katika viwanja vya Nzuguni Dodoma kuna Mengi ya Kujifunza kwa wakulima, wafugaji na wananchi wa kawaida, leo nimekutana na Dume la Ng’ombe aina ya Borani lenye umri wa Miaka 4 huku likiwa limezalisha zaidi ya majike 206.

Kwa Mujibu wa Afisa Mifugo wa Halmashauri ya wilaya ya Singida, Adam Sungita akimuelezea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema kuwa Ng’ombe huyo ana uzito wa Kg 915. Ambao ni saw ana ng’ombe wa kawaida watatu mpaka wanne.

Amewezaje kuzalisha idadi kubwa ya majike kwa kiasi hicho, Sungita anasema kutokana na Muonekano wake wa kuvuti, uwezo wa kupanda majike, uzito na ukubwa wa umbo lake vimekuwa ni vivutio tosha kwa wafugaji wilayani Singida na wale wa mikoa Jirani, ambapo wengi majike wanayofuga yanapofikia joto la kupata Mimba huwapeleka kuwapandisha na hakikia nao wamefaidika kuipata mbegu hiyo.

Afisa huyo anasema wafugaji wengine Bado hawajachelewa maana Borani huyo  ndiyo kwanza anaingia kwenye Ushebabi wa Ujana hasa akiwa na nguvu za kutosha kupanda majike, hivyo wafike tu wakamshuhudie kwenye mabanda ya Wizara ya Mifugo yaliyopo nane nane, wakamuone lakini pia wakapate Elimu kuhusu faida ya kufuga aina hiyo ya Ng’ombe ambaye ni wa nyama ambapo nyama yake inatajwa kuwa ni tamu na lainiiiii.

Sangita anasema anajivuni kwenye wilaya hiyo anayofanyia kazi wafugaji Zaidi ya 40 wamefaidika kwa kubadilisha Maisha kutokana na ufugaji wa kisasa huku wakipiga hatua za kimaendeleo katika Maisha yao na hata Borani huyo anafugwa na mtu binafsi wala si taasisi.

“Mhe. Mkuu wa Mkoa Ng’ombe huyo kwa sasa anauzwa 12 mil. Kwa mtu atakayemuhitaji”, amesema


 

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG