..........................
NA JOHN ISRAEL, NANE – NANE DODOMA
IKIWA zimesalia Siku mbili ili Darisha la
Usaili kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na Masomo ya vyuo vikuu mwaka 2024/25
kufungwa, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Kimewaalika kufika kwenye Banda lao
lililopo katika Viwanja vya maonyesho ya Wakulima na Wafugaji Nane-nane Jijini
Dodoma ili kupata ushauri.
Akiongea na Waandishi wa Vyombo
mbalimbali vya Habari katika banda hilo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano
na Masoko wa Chuo hicho Rose Joseph, amesema Dirisha la Usaili lilifunguliwa
Julai 15, na kwamba litafungwa Agosti 10, mwaka huu, hivyo kuwataka wanafunzi
wanaotaka kujiunga na masomo katika chuo hicho kuchangamkia fursa ya maonyesho
ya Nanenane kwa kufika katika Banda lao ili kupewa ushari kabla ya kufanyiwa usaili.
Amesema wanafunzi wanapewa ushauri wa kozi
za kusoma UDOM, kutokana na Ufaulu walio nao.
“tunawahamasisha watanzania wanaotaka
kuja kujiunga na masomo katika chuo cha UDOM, kuja kwenye Banda letu ili wapewe
ushauri wa kitaalam wa kozi za kuchukua kutokana na ufaulu walio nao, katika
ngazi za kuanzia stashahada hadi shahada za uzamimu”, amesema na kuongeza.