BANDA MEDIA BLOG

TALIRI YAONYESHA JIWE LISHE LA MIFUGO, NANE NANE DODOMA

 

NA JOHN ISAREAL, NANE-NANE DODOMA

TAASISI ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), imekita kambi katika viwanja vya Nanenane Nzuguni jijini Dodoma, ikiungana na mataasisi mengine kutoa elimu ya Teknolojia na bunifu mbalimbali za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi ambapo imetambulisha jiwe lishe la Mifugo lililobuniwa miaka 5 iliyopita.

Akimuelezea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule aliyetembelea na kujionea Teknolojia mbalimbali za Kilimo na ufugaji katika Mambanda ya Wizara ya Mifugo yaliyosheheni Wataalam mbalimbali, Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Prof. Erick Komba amesema jiwe hilo lipo tofauti na mawe mingine ya madini na kwamba limetengenezwa maalum kwa ajili ya nyakati za ukame

Prof. Komba amesema jiwe hilo lina mlo kamili wa mifugo kama Ng’ombe na mbuzi na kwamba lina protini, linaongeza nguvu na pia lina madini ya aina mbalimbali

Amesema kuwa lengo la kutengenezwa kwa jiwe hilo linalotengenezwa katika kituo kilichopo huko wilayani Kongwa mkoa wa Dodoma, ni kwa ajili ya kukabiliana na Uhaba wa malisho ya mifugo kipindi cha ukame.

“jiwe hili lina kilo 3, serikali imetoa ruzuku kwa wafugaji ambapo kwa sasa linapatika kwa sh. 4,000 garama ya teknolojia, linatumika siku 8 kwa ng’ombe mmoja”, amesema

Aidha amesema Taasisi hiyo imesajili ana 5 za mbegu za malisho ambazo zinatarajiwa kuwa madukani kama ilivyo kwa aina nyingine za mbegu, lengo likiwa kila mfugaji amiliki shamba  na kulima malisho yake mwenyewe.

Amesema kuwa huo ni muelekeo wa Wizara ya Mifugo wa kutaka kila mkulima alime malisho yaliyoboreshwa yenye tija. 

  Kwa Upande wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Senyamule  Senyamule aliyetembelea Mabanda ya maonesho ya Wizara za Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi amesema teknolojia zinazooshwa hapo ziwafikie wananchi ili kuleta tija kwa mnyororo wa thamani kwa mazao ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Maonesho ya Nanenane Kitaifa Kanda ya Kati 2024, yanaongozwa na kauli mbiu ya "Chagua viongozi Bora wa Serikali za mitaa kwa maendeleo endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi"

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG