NA JOHN ISAREAL, NANE-NANE DODOMA
SERIKALI imeombwa kutupia jicho Sekta ya Ufugaji wa
Nguruwe kwa kuanzisha BBT ya mnyama huyo ambaye anatajwa kuwa na nyama pendwa
Duniani kote.
Akioangea na waandishi wa Habari Katika viwanja vya
Nane- nane jijini Dodoma Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji wa Nguruwe hapa
nchini (TAPIFA), Doreen Maro amesema imefika wakati ambao serikali inatakiwa
kuitupia jicho sekta hiyo ambayo inaweza kuwatoa vijana haraka kwenye harakati
za kiuchumi.
Bi. Doreen anasema kutokana na Ufugaji Bora wa
Nguruwe mnnyama huyo anaweza kuzaa mpaka
mara Tatu kwa Mwaka ambapo kwa Uzao Mmoja huzaa kati ya vitoto 15 hadi 20 ambapo kwa kipindi cha
Miezi 6 nguruwe hufikisha uzito wa Zaidi ya Kilo 120.
“ufugaji wa kisasa wa nguruwe unalipa kwani kwa mwaka
nguruwe mmoja anazaa vitoto kati ya 30 mpaka 60 kwa kuzaa mara tatu na ndani ya
miezi 6 nguruwe hufikisha kilo 120 ambayo ni biashara inayolipa sana”, amesema
Amesema Mbegu bora ya nguruwe inayotoka nje ya nchi
inapatikana kwa garama ya kati ya 500,000 na 600,000 hivyo kwa mfugaji mdogo si
rahisi kumudu hivyo kama serikali ikitia mkono itawafanya wengi wanaotamani kujiunga
na ufugaji wa mnyama huyo mwenye nyama pendwa Duniani kote.
Pia amewakaribisha wakazi wa Dodoma na mikoa Jirani wanaotembelea
katika Viwanja vya Nane- nane wafike katika mabanda ya Mifugo husan kwenye
ufugaji wa Nguruwe ili wakajipatie elimu ya ufugaji bora wenye tija.
Mnufaika ambaye ni mmiliki wa Shamba la Mbegu za Nguruwe
la Marangu, Julieth Tarimo amesema katika ufugaji wanazingatia ubora ndiyo
maana hata radha ya Nyama ya mnyama wanaefuga wao ni tofauti kwani haina
mafuta, wala Shombo
“nguruwe wetu wanalala sehemu nzuri, wanakula chakura
chenye ubora ambacho siyo makombo,wanakunywa maji ya bomba, niseme tu
tunazingatia ubora katika ufugaji ndiyo maana nyama yake haiana shombo, mafuta
wala haikinaishi”, amesema
Amewataka pia vijana wachangamkie kila fursa
wanayoipata badala ya kusubiri ajira pekee.







