BANDA MEDIA BLOG

WANANCHI WAKOSHWA NA BIDHAA ZA KINGLION NANE - NANE DODOMA

 

NA JOHN BANDA, NANE-NANE DODOMA

WANANCHI waliotembea Maonyesho ya Kilimo na Mifugo yaliyofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma Wamekoshwa na Bidhaa Mpya zilizoonyeshwa na Kampuni ya KINGLION

Meneja Mauzo wa kampuni hiyo inayotengeneza na Kusambaza Pikipiki, Mabati na Maguta ya kubebea mizigo, Joseph Banzi akiongea kwenye banda lao la maonyesho  nanenane amesema wananchi hao wamevutiwa na Bidhaa walizoonyesha.

Amesema Kampuni hiyo pia imetambulisha Bidhaa Mpya ya Water Pump na Jenereta  Pamoja na Pikipiki mpya Kinglion 110 ambayo inatumia lita moja ya mafuta kwa umbali wa km. 70 ambayo tenk lake lina ujazo wa lita 13 kwa wakati mmoja.

“kwa kweli wananchi wengi wametutembelea na kuvutiwa na bidhaa zetu, wapo waliovutiwa na pikipiki, mabati, maguta, Pikipiki mpya Pamoja na Water Pump na Majenereta”, amesema Banzi

hata hivyo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akihitimisha sherehe hizo za nanenane alitangaza kuwaongezea Wananchi siku mbali zaidi ambapo maonyesho hayo yatahitimishwa agosti 10 siku ya jumamosi na kwamba huduma zote zitaendelea kutolewa kama kawaida.






Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG