BANDA MEDIA BLOG

Ally Kamwe Azidi Kuwavuruga Simba

 Ally Kamwe Azidi Kuwavuruga Simba

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Ali Kamwe amefichua mipango ya klabu hiyo ambapo ameeleza kuwa Januari kutakuwa na ongezeko la mchezaji mwingine wa kigeni ndani ya kikosi hicho ambacho mpaka sasa tayari ni moto wa kuotea mbali.

“Nataka niwaambie tu Yanga hii bado, Januari kutakuwa na ongezeko la mchezaji mwingine wa kigeni. Kwa hiyo haijakamilika, tunahitaji kuchukuwa ubingwa wa Afrika,” —amesema Ali Kamwe

“Huyo mchezaji aliyemsema Rais Hersi tumemleta alikuwepo uwanjani katika mchezo wa Dabi ya Kariakoo na amekuja kufanya mazungumzo na kusajili tayari kwa kuanza kazi katika michuano ya kimataifa,” amesema Kamwe.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG