BANDA MEDIA BLOG

MAVUNDE ATOA SIKU SABA UMEME UWAKE MACHINGA COMPLEX

                    ................................

              NA JOHN BANDA, DODOMA

MBUNGE wa jimbo la Dodoma mjini Athony Peter Mavunde amemuagiza Mkurugenzi wa jiji hilo kuhakikisha anaweka Pevin (Mtomo) kwenye barabara ya vumbi ambalo kwa kiwango kikubwa limeathili muonekana wa soko hilo Pamoja na Bidhaa za wafanyabiasahara

Pia amemuagiza Mkurugenzi wa Tanesco, mkoa wa Dodoma kuhakikisha anatatua kero ya Umeme ambayo imekuwa ikiwakabiri wafanyabiasahara hao kwa kipindi cha siku saba.

Mhe. Mavunde, ametoa agizo hilo wakati akiongea na wafanyabiashara wadogowadogo maarufu Wamachinga, kwenye mkutano wao wa kwanza wa kuwatamburisha viongozi wapya waliokabidhiwa nafasi hizo hivi karibuni kutokana na Meneja Pamoja na Mwenyekiti wa soko hilo, kutumbuliwa na Mkuu wa Mkoa huo hivi karibuni kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo ubadhilifu.

Mavunde ambaye pia ni Waziri wa Madini amesema maelekezo ya Serikali aliyopewa mkurugenzi wa jiji, baada ya kamati ya Bunge kutembelea Soko hilo ni kuwa barabara hiyo iwekwe vigae kwa ajili ya kuondoa vumbi kubwa linalotimka na kuharibu muonekano wa soko Pamoja na kuathili bidhaa za wafanyabishara hao.

“Pamoja na kuhakikisha Pevin kwenye barabara, Mkurugenzi wa jiji na wewe wa Tanesco hakikisheni mnatatua kero ya ukosefu wa Umeme, kwenye baadhi ya vizimba ndani siku saba na si vinginevyo, sijui mtafanyaje lakini staki kusikia wafanyabiashara wanaendelea kutaabika kwa kukosa umeme”, amesema

Aidha Mbunge huyo aliwachangia kiasi cha Milion 10 kwa ajili ya kuendeleza mfuko wa kusaidiana wa Machinga hao pamoja na kugawa mitungi ya Gesi 47, bure kwa mama na baba lishe wa sokoni hapo.

Jabir Shekimweri Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, amewapongeza Uongozi mpya kwa kuja na mpango wa kuanzisha mfuko wa kuweka na kukopo Pamoja na kusaidiana.

“leo nimefurahishwa sana kwa hili mlilolianzisha la mfuko ambalo najua litawasaidia sana, niwapongeze sana viongozi na niwahakikishie Ushirikiano na serikali”, amesema

Aidha amesema nguvu ni kitu kinachoisha haiwezekani mtu kuwa na miaka 70 na kuendelea na bado akawa anafanya umachinga,kutokana na furaha hii ofisi yangu itachangia 2 mil. Lakini pia “hakikisheni ndani ya miezi mitatu hamtoi fedha kwenye akaunti mpaka mjiwekee mfumo mzuri wa usimamizi wa fedha kisha mtuletee tuuone”. amesema

 Mmoja wa Machinga sokoni hapo Othman Mhanga amemuomba Mbunge kuwashika mkono kwa kuwachangia kiasi cha fedha kwa ajili ya kuanzisha mfuko wa kusaidiana, ambapo amesema anatamani mfuko huo ukue kiasi cha kufikia kuanzisha Saccos ambayo itawasaidia kukopeshana badala ya kuendelea kunyanyaswa na taasisi za mikopo

Viongozi wa soko la Machinga Complex jijini Dodoma, waliotamburishwa ni Kaimu Mwenyekiti Nyamageni Kingamkono wakati katibu wake ni Simon Mhagale huku kukiwa na mabalozi wa vizimba vya wafanyabishara kutokana na aina za biashara zao. 















Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG