BANDA MEDIA BLOG

MWENGE WARIDHISHWA NA MIRADI YA MAENDLEO YA BILIONI 2.104 ILEMELA

 

Bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ye Msingi Buswelu lililozinduliwa leo na Mwenge wa Uhuru.

Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation, Alhaji Dkt.Sibtain Meghjee,akizungumza leo kabla ya Mwenge w Uhuru kuzindua mradi wa maji uliotekelezwa na taasisi hiyo katika Shule ya Bwiru Sekondari (Wavulana) ikishirikiana n Manispaa ya Ilemela.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Godfrey Mzava (wa nne kutoka kulia), akizungumza leo kabla ya kuzindua mradi wa maji, Bwiru sekondari (Wavulana)
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru,Godfrey Mzava (wa kwanza kutoka kushoto),leo akifungua mradi wa maji leo katika sekondari ya Bwiru Wavulana, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masalla na wa kwanza kutoka kulia ni Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation,Alhaji Sibtain Meghjee. Picha zote na Baltazar Mashaka
…………
NA BALTAZAR MASHAKA, ILEMELA
MWENGE wa Uhuru umeridhishwa na miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika Wilaya na Manispaa ya Ilemela yenye thamani ya sh.bilioni 2.104 katika sekta ya afya, elimu, maji,biashara na mazingira.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024,Godfrey Mzava amesema leo, baada ya kuweka jiwe la msingi katika wodi ya Mm na Mtoto katika Zahanti ya Nyakato, wilyani Ilemela.

Amesema katika miradi yote Mwenge ulikopita kuweka mawe ya msingi,kukagua na kufungua baadhi,umeridhika kwa namna ilivyotekelezwa kwa ubora na kwa usimamizi mzuri, hivyo wameitendea haki fedha ya serikali,michango ya wananchi na wadau wa maendeleo.

“Kote tulikopita kwenye miaradi,tumekuta wananchi wamejitokeza kwa wingi kuja kuulaki Mwenge wa Uhuru lakini pia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.Nakupongeza wewe kiongozi wetu wa shughuli za serikali wilayani kwetu kwa namna ulivyoyaunganisha makundi ya kijamii na kisiasa, ndio maana miradi ya maendeleo imefanikiwa,”amesema Mzava.

Amesema mafanikio ya utekelezaji wa miradi hiyo unadhirisha Ilemela  anapewa ushirikiano wa kutosha na viongozi wengine wilayani huko, watumishi na wananchi.

“Tumeona utekelezaji wa miradi  ya maendeleo, ni dhahiri tusingeweza kupita katika miradi yote kazi inayofanywa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025,ni imani yetu kuwa miradi yote imetekelezwa kwa viwango na ubora ule ule,”amesema Mzava.

Mwenge huo wa Uhuru uliweka jiwe la msingi katika jengo la wodi ya Mama na Mtoto la Zahati ya Nyakato lililogharimu sh. milioni zaidi ya 227.9 za serikali kuu, mapato ya ndani na wananchi,pia umefungua  bweni la watoto wenye mahataji maalum katika shule ya Msingi Buswelu,lililogharimu sh. milioni 172 zikiwemo za mapato ya ndani na serikali.

Aidha umezindua mradi wa maji katika shule ya sekondari Bwiru wavulana, uliojengwa kwa gharama ya sh. milioni 31.548 kwa ushirikiano kati ya The Desk & Chair Foundation (sh.milioni 19.75 na halmashauri ya Ilemela sh. milioni 11.798 za mapato ya ndani),

Mwenge wa Uhuru pia umezindua shule ya sekondari Kisenga iliyogharimu milioni 584.28 na mradi wa Klabu ya Wapinga Rushwa katika shule hiyo wenye thamani ya sh. milioni 380,kituo cha mafuta cha GBP kilichogharimu sh.milioni milioni 520 na barabara ya Kiyungi sh.milioni 499.655.

Pia umekagua miradi ya upandaji miti wenye thamani ya sh.3.9 pamoja na wa matofali wa kikundi cha Community Vision wenye thamani ya sh.milioni 60 ilikaguliwa na kufanya jumla ya miradi yote kugharimu sh. bilioni 2.104.
Naye Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation, Alhaji Dk.Sibtain Meghjee, amesema anatambua ushirikiano ulipo kati ya taasisis hiyo na serikali katika kuhudumia jamii.
“Tunashukuru serikali kwa ushirikiano inaotupa  na kutuwezesha kutekeleza miradi ya kuihudumia jamii katika sekta za elimu, afya na maji, ni mara ya tano Mwenge kukagua ama kuzindua miradi tunayotekeleza,”amesema na kuongeza kuwa mradi huo wa kisima kirefu una uwezo wa kuhudumia wanatu 3000 kwa mwaka.
Kwa Upande wake Mbunge wa Ilemela (CCM), Dkt.Angeline Mabulaaamesema serikali imetoa sh. bilioni 78.2 za miradi ya maendeleo ambapo sekta ya maji ilipata sh.bilioni 71. za chanzo cha Butimba,mradi wa Igombe sh.milioni 869 na wa matokeo ya haraka sh.bilioni 4.4 , sekta ya elimu bilioni 8.4 za elimu bila malipo na bilioni 19.za miundombinu.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG