BANDA MEDIA BLOG

POLISI YASHTUKIA UKIMYA WA WANAOIBIWA MIFUGO IYUMBU YATOA USHAURI HUU

Polisi Kata wa Kata ya Iyumbu jijini Humo, Daudi Matala akifafanua jambo kwenye mkutano huo, 

                                             ........................

                                       NA JOHN BANDA, DODOMA

JESHI la Polisi limewataka wakazi wa Kata ya Iyumbu, jijini Dodoma kutoa Taarifa za Uhalifu na wahalifu ambao umekua ukifanyika katika Kata hiyo Mara kwa mara ambao umekuwa ukiwasababishia hofu wananchi na Mali zao

Wito Huo Umetolewa na Polisi Kata wa Kata ya Iyumbu jijini Humo, Daudi Matala Kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Viwanja vya shule ya Msingi, ambapo amesema Wizi wa mifugo, Uuzaji, Usafirishaji na uvutaji wa Bangi vimekithili.

Amesema matukio ya wizi hasa wa mifugo yamekua yakitokea mara kwa mara lakini cha kushangaza haoni wahusika wanaoibiwa kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi, ambapo amesema Hali hiyo ina ishara mbaya.

"Inashangaza kusikia taarifa za mifugo kuibiwa wiki kwa wiki hapa iyumbu toka kwa wasamalia wema, huku wahusika walioibiwa hawatoi taarifa polisi, Hali hii ina kiashiria cha hatari maana huwezi kujua miyoni mwao wanawaza nini", amesema

Aidha amesema Ulifu wa Aina nyingine uliokidhili katika Kata hiyo ambao jeshi Hilo linapata taarifa za Kiintelejensi ni uuzaji, usafirishaji na uvutaji wa Madawa ya kulevya ikiwemo Bangi.

"Kupitia kampeni ya familia  yangu haina uhalifu,  nitoe wito Kwa wakuu wa Kaya kuhakikisha kuhakikisha familia zao hazina watu wanaofanya uhalifu, kwani wanaofanya vitendo hivyo ni watoto wenu na wengine katika familia", amesema na kuongeza Afande Matalani

Awali akiongea katika mkutano huo, Diwani wa Kata ya Iyumbu Eliasi Sutuchi ameliomba jeshi la polisi kuingilia Kati vitendo vya uhalifu huo vinavyotoke kwani mpaka sasa Zaidi ya Ng'ombe 80, mbuzi 24 huku 16 zikiibiwa wiki ilipita.

Nae Mtendaji wa Kata hiyo Stanley John ameainisha Changamoto nyingine zinazoikali kata hiyo, kuwa ni pamoja na Ukosefu wa Nyumba za Walimu wa shule ya sekondari, upungufu wa nyumba za walimu Msingi, ukosefu wa shule za msingi katika mitaa ya mbali, Ukosefu wa nyumba ya Daktari wa zahanati, Upungufu wa maji baadhi ya maeneo, ukisefu wa umeme baadhi ya maeneo, madaraja ya kuunganisha Udom, Nyere, Udom, Iyumbu na mwinyi na maeneo mengine, Barabara ya kiwango cha lami, baadhi ya maeneo hayajafunguliwa Barabara, kusua sua kwa ziezi la umilikishahi ardhi,  ukosefu kituo cha afya na kituo cha 
Katibu wa Diwani Jumanne Chapembe akizungumza jambo kwenye mkutano mkuu









Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG