BANDA MEDIA BLOG

UNYANYASAJI KIKWANZO KWA WANAWAKE KUWANIA NAFASI YA UONGOZI

 

MKURUGENZI Chama cha waandishi wa habari  Wanawake  (TAMWA ZNZ),  Dk.Mzuri Issa amesema bado kuna changamoto zinazowakwamisha Wanawake kuwa viongozi ikiwemo unyanyasaji wa kundi hilo mtandaoni.

Akifungua mkutano wa wadau wa masuala ya wanawake na uongozi  kupitia vyombo vya habari  huko  Ofisi za TAMWA  Tunguu  alisema hatua hiyo inachangia kuwavunja moyo na kuwarudisha nyuma Wanawake kugombea nafasi hizo.

“Bado kuna  udhalilisha na irudishwaji nyuma wa Wanawake kugombea nafasi za uongozi ikiwemo  kuogopa, kukatishwa tamaa, kukatazwa , na kukemewa kushiriki harakati za kisiasa” alisema Dk.  Mzuri

Alisema lengo la chama hicho ni kuona haki za Wanawake wzinaimarishwa  kwa njia mbali mbali  ikiwemo kuwekewa mifumo ya kuwalinda kipindi cha  siasa na itakayowawezesha  kugombania nafasi za uongozi na kushinda.

Aidha alieleza kuwa chama hicho kinatamani kuona wanawake wananyanyuliwa na kuwekea mazingira mazuri ya kuwa   salama mtandaoni  wanaposhiriki katika nafasi za uongozi ili  kufikia usawa wa 50 kwa 50.

“Watu wasiojiamini huandaa mikakati ya kuwarejesha nyuma wanawake wenye nia ya kugombea nafasi za  uongozi hivyo ni mwiko kuzungumzia masuala ya kurudi nyuma  katika kufika usawa wa 50 kwa 50”. Alisema Dk. Mzuri

Afisa elimu kutoka Mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu uchumi ZAECA Yussuf Juma Suleiman alisema   wanawake wana nafasi sawa na wanaume kushiriki katika uongozi hivyo ni vyema kila mmoja kuchukuwa hatua kuhakikisha usawa katika nafasi za uongozi unapatikana.

Alifahamsha kuwa moja kati ya vikwanzo  vinavyowarudisha nyuma  wanawake katika kugombea nafasi za uongozi ni rushwa ya ngono ambapo sheria ya rushwa namba 5 ya mwaka 2023, kifungu cha 53 imeeleza mazingira ya ngono hivyo ni vyema wanawake kuyajua mazingira hayo ili kuwa mstari wa mbele kuzuia na kupambanana vitendo hivyo visitokee.

“Kabla wanawake hawajaingia katika kugombea nafasi za uongozi, ni vizuri kupewa elimu ya uraia, ili kujua miiko na misingi ya uongozi, ili wasiwe mwanya wa kutoa rushwa.” Alisema ofisa huyo

Ofisa sheria mwandamizi Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa Abdulrazak Said Ali,  aliwataka wanawake kuwa na imani na ofisi hiyo  kwani tayari imeanzisha dawati la jinsia kushuguhulikia masuala ya  jinsia bila ya upendeleo wowote.

Wadau walioshiriki katika  mkutano huo akiwemo Mwatima Issa Rashid na Nusra Shabani walisema uzowefu unaonesha kuwa changamoto ya uchumi bado inawarudisha nyuma  wanawake kufikia malengo ya dhamira ya mwanamke kuwa kiongozi hivyo  kuvitaka vyama vya siasa  kuandaa Sera zitakazowewezezha Wanawake kiuchumi ikijumuisha kuweka  mafungua maalum ya wanawake ili kuwasaidia kufikia malengo yao.

Aidha waliishauri  ZAECA kutoa  elimu ya kutambua mazingira ya rushwa ya ngono ila kujikinga na kuzuia kutokea kwa vitendo hivyo na kuwataka kuweka wazi Sheria za adhabu kwa wanaodhalilisha wanawake kupitia mitandao .

“Kuna haja ya kuwapatia Wanawake elimu ya uraia na stadi za maisha  ili waweze kujitambua na kuepukana na kutumika vibaya na kuwa myanya ya rushwa ya ngono” walishauri wadau hao.

Hata hivyo waliishauri TCRA kuzuia taarifa zinazomvunjia uaminifu mwanamke kwa jamiii ili kuwa huru kutumia mitandao hiyo  kwani mwanamke mtetezi lazima awe salama mtandaoni.

TAMWA ZNZ imeandaa kikao hicho kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wa taasisi za Serikali na binafsi pamoja na waaandishi wa habari vijana ili kuwajengea uwezo wa kuandika na kuzifanyia uchambuzi habari zinazohusu wanawake na uongozi kupitia mradi wa wanawake na uongozi.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG