NA JOHN BANDA, DODOMA
MKUU wa wilaya ya Dodoma mjini Jabir Shekimweri amewataka wamiliki wa Shule za kulelea Watoto (DAYCARE CENTRE’S) kutimiza
vigezo vilivyomo kweye usajili ikiwemo kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya usalama
wa watoto.
Pia wahakikishe wanafanya kazi zao kwa kushirikiana
na serikali badala ya kuwafanya baadhi ya Maafisa maendeleo ya jamii kuwa
maadui.
Shekimweri ameyasema hayo wakati akiongea na wamiliki,
walezi na walimu wa shule za awali waliokutana kwenye hafla ya kufahamiana na
kubadilishana uzoefu Pamoja na kuzijadili changamoto zinazowakabili
Amesema jambo la msingi kwa wamiliki ambao bado
hawana usajili ni kusajili vituo vyao, ambapo ili kupata usajili huo lazima wapite na kupata
utambulisho toka kwa viongozi wa serikali za mitaa wanakofanyia kazi.
Kabla ya kukaguliwa hakikisheni mnaweka mazingira
mazuri kwa ajili ya usalama wa watoto
“Vituo hivi vipo kwenye mitaa, hakikisheni mazingira
yake yanakuwa katika hali ya usafi ili kuepuka magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu
na magonjwa mengine, lakini pia usalama wa Watoto na walezi wao kutokana na
vibaka”, amesema
Aidha Shekimwel amesema ili kufanya urahisi wa
utendaji wa kazi wahakikishe wanafanya kazi karibu na serikali.
“kuna baadhi ya wamiliki ambao wamekuwa wakiwachukulia maafisa maendeleo ya jamii kama maadui wasiowatakia mema katika kazi zao lakini niwaambie tu hao walisomea fani ya malezi ya Watoto na wanapokuja kuwakagua msidhani ni wao bali taratibu za serikali mkitmiza vigezo haita wasumbua”, amesema
Awali Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wamiliki wa Vituo vya
Kulelea Watoto (DAYCARE CENTRE’S) Dodoma, Rehema Mdengede amesema wamekutana
katika khafla hiyo kwa ajili ya kufahamiana, kuzijadili changamoto
zinazowakabili, Pamoja na kubadlishana uzoefu katika utendaji wao wa kazi,
ambapo wadau mbalimbali wameshiriki Pamoja na serikali.