BANDA MEDIA BLOG

WATANZANIA WATAKIWA KUZITUMIA HUDUMA ZA USAFIRI WA ANGA KWA WINGI KWANI SIO ANASA

 


Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya viwanja vya ndege Tazania ,Abdul Mombokaleo katika banda la mamlaka hiyo ambao wamehudhuria kongamano mkoani Arusha .

 Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo ,Abdul Mombokaleo akitoa maelezo kwa Waziri wa uchukuzi Prof.Makame Mbarawa katika banda lao mkoani Arusha.

………………..

Happy Lazaro,Arusha .

WATANZANIA wametakiwa kuzitumia kwa wingi  huduma za  usafiri wa anga  kwani sio anasa   kwani serikali inajitahidi  kujenga viwanja zaidi na kuboresha miundombinu, hivyo itakuwa haina  maana kama wananchi watakuwa hawajapata  hamasa  ya kutumia viwanja vya ndege. 

Aidha wametakiwa kutumia ndege zetu na miundombinu yetu kwa faida ya ujumla kwani wanapokuwa wengi katika matumizi inawapa  wao  sababu ya makusudi  katika kupunguza  gharama kwani wakiwa wengi wanaweza  kushusha gharama.

Hayo yamesemwa mkoani Arusha na   
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya  viwanja vya ndege Tanzania ,Abdul Mombokaleo wakati akizungumza kwenye Kongamano la sekta ya mawasiliano na usafirishaji linaloendelea  mkoani Arusha. 

Amesema kuwa ,kwa ujumla maeneo ambayo wanaangalia ni  ubora wa biashara zao na  biashara kwa ujumla .

Aidha amewataka wananchi waelewe  kuwa matumizi ya  shirika la ndege sio luxury  bali ni moja  ya njia ambayo inaharakisha harakati za kiuchumi kutoka sehemu  moja kwenda nyingine ndani ya muda mfupi na ukafunga biashara yako na kurudi kwa muda mchache ,hivyo kuwataka kutumia huduma hiyo kwa wingi ili kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla .

“Maeneo ambayo tumeyapa  kipaumbele ni kuangalia jinsi ya kuboresha   zetu na kuboresha bei  na gharama kwa ujumla katika maeneo yote .”amesema .

“Tumechukua changamoto kutoka kwa Waziri wa uchukuzi ,Prof .Makame Mbarawa  kuwa tukakae chini na kuangalia namna ya kuboresha huduma hii  sambamba na kuwa na huduma nzuri ambayo itawavutia watoa  huduma kuja kutumia viwanja vya ndege.”amesema Mombokaleo.

Amesema kuwa,serikali inafanya jitihada kubwa sana katika kuongeza idadi ya viwanja kwa ubora wa hali ya juu na hivyo wao kuwapa changamoto au chachu ya kuweka miundombinu mizuri ya kuvutia  watoa huduma mbalimbali ili kuwe na mantiki ya kutumia  viwanja hivi vinavyojengwa na serikali kwa nia njema.

Akizungumzia hali ya viwanja kwa sasa amesema kuwa,  kuna viwanja ambavyo vinaendelea kuboreshwa zaidi kwa maana ya kuongeza mifumo  ili iwe ya kisasa na kuweza  kukidhi viwango vya kimataifa kama ilivyo kwa nchi zingine. 

Amefafanua kuwa ,kuna  miradi  inaendelea sasa hivi  ya ujenzi wa viwanja vipya vya ndani na kuboresha kwani wanataka sekta ya anga pia kuwa  kama sekta ya usafiri wa magari na meli kwamba kuwe na option nyingi kwa abiria .

Amesema kuwa tutaangalia eneo  zima  kwa maana ya abiria ,mizigo na huduma mbalimbali kwa kupitia anga  japo inaonekana usafiri wa anga ni huduma ya gharama lakini malengo ya serikali ni kuifanya huduma hii iwe nyepesi na iwe na mvuto kwa wananchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG