BANDA MEDIA BLOG

WAZAZI WATAKIWA KUTOWAPANGIA WATOTO FANI ZA KUSOMEA .

 Mbunge wa jimbo la Tarime , Mwita Chacha ambaye pia ni Mkurugenzi wa shule za Gati memorial na Nyahiri akizungumza katika mahafali hayo mkoani Arusha .

Wahitimu wa darasa la saba wakitumbuiza katika mahafali ya darasa la saba katika shule ya mchepuo wa kiingireza ya Gati Memorial iliyopo mkoani Arusha
Happy Lazaro,Arusha .

Arusha.Wazazi  wametakiwa kutowapangia  watoto wao fani za kusoma kwani kwa kufanya hivyo wanawakatisha tamaa ya kufanya kile wanachokipenda kwa maisha yao ya baadaye.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa jimbo la Tarime , Mwita Chacha ambaye pia ni Mkurugenzi wa shule za Gati memorial na Nyahiri zilizopo  mkoani Arusha  wakati akizungumza katika mahafali ya 11 katika.shule ya  mchepuo wa kiingireza ya Gati Memorial iliyopo mkoani Arusha .
Amesema kuwa, kumekuwepo kwa changamoto kubwa ambayo inalalamikiwa na watoto walio wengi  kuhusu wazazi kuwapangia  fani za kusoma jambo ambalo linawakatisha tamaa ya kufikia ndoto zao.
“Kila mtoto ana malengo yake  ya kuwa mtu fulani katika maisha yake ya baadaye  hivyo wanavyosoma wana matarajio  yao sasa mnapowapangia  tena kozi ya kusoma mnakatiza  ndoto zao za baadaye kwa kusomea fani  wasizozipenda jambo ambalo linawakatisha tamaa sana .”amesema Mwita .
Aidha amefafanua zaidi  kuwa,wapo wahitimu wengi ambao wamehitimu vyuo vikuu  na wamesomea kazi ambazo  hazikuwa  chaguo lao imewabidi  wasome  tu kutokana na kushinikizwa na wazazi wao  ila sio kwa kupenda wao wenyewe. 
Amefafanua zaidi kuwa,ni lazima wazazi wawape nafasi watoto wao  wachague  kile moyo wao unataka na sio wazazi kuwachagulia maana mwisho wa siku inasababisha kuwa  na wataalamu wasioipenda  kazi yao .
“Ili tuweze  kupata wataalamu wenye moyo zaidi tuwaache tu  wasomee  kile wanachokipenda kuliko kuwachagulia  fani ambazo haziendani na wanachohitaji  wao.”amesema  Chacha.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo , Beatha Shirima amesema kuwa wamekuwa wakiwajengea  watoto mazingira ya kuweza kujitegemea wenyewe na kuweza kuwa viongozi wa kesho. 
Aidha alitumia fursa hiyo kuwataka wazazi kuendelea kuendeleza nidhamu ya watoto hao ambayo walikuwa nayo tangu wakiwa shuleni ili waendelee kuitangaza shule hiyo.
Kwa upande wa wanafunzi katika.mahafali hayo ,wameipongeza shule hiyo kwa namna ambavyo imekuwa ikiwaandaa  kuwa viongozi bora  wa baadaye kwa kuwafundisha namna ya kuweza kujiamini  na kuwa viongozi bora  wa kesho pamoja na kufundishwa  masomo ya ujasiriamali ili waweze kujiajiri  wao wenyewe.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG