.......................................
Na Rose Jacob,MWANZA.
NAIBU waziri wa Wizira ya Uchukizi David Kihenzile ,amezindua jina jipya na nembo ya Kampuni ya Meli Tanzania,kutoka Kampuni ya Huduma ya Meli na kuitwa Kampuni ya Meli Tanzani,(TASHICO) au Tanzania Shipping Company.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi,Makame Mbarawa,katika hafla fupi ya uzinduzi huo,Kihenzile,amesema hatua ya kubadilisha jina ni mhimu sana katika kuimarisha miundombinu ya kusafirisha shehena za mizigo,hivyo TASHICO inapaswa kuweka mipango thabiti ya kuendelea kimarika.
"TASHICO ni kiungo mhimu ambacho akinafanyishughuli zake ndani ya Nchi tu,bali hadi Nchi jirani,serikali inaendelea kufanya uwekezaji,hivyo mnapaswa kuongeza ubunifu,kupunguza malalamiko ya upotevu wa mizigo,mara Matusi,"amesema Kihenzile.
Amesema kunabaadhi ya watendaji wanapewa dhamana ya kusimamia miradi,lakini wanaharibu fedha na kuleta miundombinu Haina kiwango,hivyo TASHICO,fedha wanazokusanya wahakikishe zinatumika kwa utaratibu na kuongezamkakati wa masoko,huku akiwataka moango wa kuongeza Meli Bahari ya Hindi ufanyike haraka maana wateja wanusubiri kwa hamu safari hizo.
Akitoa taarifa ya Kampuni ya Meli Tanzania, (TASHICO),Mkurugenzi Mtendaji Eric Hamiss,alisema kubadilishwa kwa jina la kampuni hiyo lengo ni kukua kibiashara,kuendana na dhana ya Nchi,ikiwa matarajio ni kuitamburisha Taasisi hiyo ndani na nje ya Nchi.
Amesema neno Huduma za Meli lilikuwa likiakisi Taasisi hiyo,hivyo kushindwa kupata frusa za kifedha kutoka na kuonekana wao wanatoa huduma nasiyo wafanyabiashara,hivyo mchakato wa kubadili jina hilo na nembo ulianza mwaka 2021.
"Kampuni hiyo kuanzia mwaka 2015,ilikuwa imekufa kutokana na kukosa mwekezaji,hivyo mwaka 2019 hadi 2020 ilianza kuimalika,hadi sasa Taasisi hii ina meli 18,zinazofanya kazi ni meli 8,tumefanikiwa kurudisha meli 3 zilizokuwa zimechakaa kwa sasa watumishi waliyopo ni 320 lengo letu ifikapo 2025 tunahitaji kuwa na watumishi 500,"alisema Eric.
Aidha amesema wameanza mchakato wa ujenzi wa Meli ya mizigo katika Bahari ya Hindi na ifikapo 2030 kutakuwa na Meli nne katika Bahari hiyo,huku akisema Serikari ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hasani,imewekeza zaidi ya Tilioni 1.ili kuimalisha shughuli za Meli pamoja na miundombinu.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza,Baryanda Elikana,akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda,amesema wizara iangaliye miundombinu ya usafiri wa majini na relini,kwa kuwapunguzia adha wananchi,ikiwa watakata tiketi moja atumie na melini kama anatumia Tena njia ya majini au anafairisha mzigo.
Tags
HABARI KITAIFA