BANDA MEDIA BLOG

TIMU YA WATAALAM WA UANDAAJI MPANGO KAZI KITAIFA WA HAKI ZA BINADAMU NA BIASHARA WAMEPONGEZWA


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria,ambaye pia ni Mwenyekiti  wa Kamati ya kusimamia Uandaaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara,Dkt.Franklin Rwezimula ,ameipongeza Timu ya Wataalam ya Uandaaji Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara kwa kufanya mapitio ya nyaraka mbalimbali,kukusanya taarifa kwa kutembelea maeneo mbalimbali tanzania bara na zanzibar na kufanya majadiliano na taasisi za umma,asasi za kiraia pamoja na kutumia uzoefu kutoka katika nchi jirani ili kuweza kufanikisha kuandaa taarifa ya tathmini ya haki za binadamu ikiwa ni nyaraka muhimu katika uuandaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara

Pongezi hizo amezitoa wakati wa majumuisho ya kikao cha Kamati ya usimamizi uuandaji wa Mpango huo kilichofanyika tarehe 14-15 Novemba,2024  Jijini Arusha.

Pia Dkt Franklin  ametoa shukrani kwa Shirika la Maendeleo  la Kimataifa (UNDP) na wadau wengine kwakutoa ushirikiano na kufadhili katika  hatua mbalimbali za Mchakato wa Uandaaji  wa Mpango  Kazi huo.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG