BANDA MEDIA BLOG

WARSHA ZA CCMP ZAENDELEA KUCHANJA MBUGA, MAASKOFU NA WATUMISHI WA MUNGU WANENA

 

Askofu wa Kanisa Angalikana Tanzania, Dayosisi ya Biharamulo mkoani Kagera, Vithalis Yusuph Akifafanua jambo wakati alipokuwa akifungua Warsha ya CCMP Kwa watumishi wa kanisa hilo.

                      .........................

                 NA JOHN BANDA, BIHARAMULO

VIONGOZI wa dini Pamoja  na Waumini wao wametakiwa  kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha kwa kujiwekea Akiba badala ya kutumia mpaka senti ya mwisho hali inayowasababishia kutaabika pindi inapotokea dharula ya ugonjwa au Misiba kwa wapendwa wao

Ushauri huo Umetolewa na Askofu wa Kanisa Angalikana Tanzania, Dayosisi ya Biharamulo mkoani Kagera, Vithalis Yusuph kwenye Ufunguzi wa Warsha ya siku 5 kwa watumishi wa kada mbalimbali wa kanisa hilo inayolenga kuzitambua Rasirimali na Fursa za kiuchumi ikiwa ni Pamoja na jinsi ya kuzitumia (CCMP).

Askofu Yusuph amesema sababu kubwa inayowasababisha baadhi ya Watumishi, Wakirsto na wanajamii kushindwa hata kusafiri kwa wakati pindi inapotokea Msiba au Ugonjwa kwa wapendwa wao, ni kutokana na wengi wao kushindwa kujiwekea akiba kupitia vipato wanavyovipata.

Amesema Baadhi ya Viongozi wa kanisa, wakristo na wanajamii hushindwa kujiwekea akiba wakidhani ni lazima wawe na maburungutu ya fedha ‘hapana’ “kwa mfano mimi wakati Fulani nilipokuwa nasoma nilikuwa najiunga kwenye foreni benki nikiwa na Elfu 5 au 3 kujiwekea akiba, wakati wengine wakiwa na mifuko iliyojaa noti lakini sikujali nilijua ninachokifanya ninachokifanya ni kwa ajili ya baadae yangu.

“kujiwekea akiba si kutokana na ukubwa wa kipatao unachopata bali ni utashi”, amesema

Akizungumzia Mafunzo ya CCMP, Askofu huyo amewataka wachungaji kwenda kuwasaidia watu li waondokane na Umasikini kwa kuwafundisha jinsi ya Kuzitambua Rasirimali na Frusa walizonazo kwenye mazingara yao na kuzitumia, akitoa mfano wa matikiti ambayo maiaka ya nyuma yalitumika kuwapa Ng’ombe na mifugo mingine kipindi cha uhaba wa maji, bila kujua hiyo ni rasirimali ya kiuchumi.

Ameongeza pia kwa watumishi waaonafanya kazi na kupata Mshahara ni vizuri waigeuze kuwa Rasirimali ya kuanzisha Miradi ya kiuchumi badala ya kuitumia yote huku wakiwa na matumaini ya kupokea tena mwisho wa mwezi ujao.

“hakuna mtu anayeweza kuwa Tajiri au kuwa na uchumi mzuri kupitia msahara anaoupata mwisho wa mwezi, geuzeni fedha manazopata kwenye mishara kuwa fursa za kujiendeleza kiuchumi badala ya kuzitumbua zote huku mkisubiri kupokea mwezi mwingine”, amesema

Kwa Upande wake Mkuu wa Chuo cha Biblia Mkoani Morogoro, Kasisi Samweli Maduma amesema Mungu alipomuumba Mwanadamu na kumuweka kwenye Dunia yenye kila Rasilimali alitaka aishi Maisha ya Utosherevu

“kwenye Bustani ya Edeni kulikuwa na ardhi, mito, miche izaayo matunda na madini ya aina mbalimbali hizo zote ni rasilimali za kumfanya mtu aishi Maisha ya utosherevu kubwa ni kuzitambua na kisha kufanyia kazi ili tuweze kuyafikia maendeleo ya kiuchumi”, amesema

Kasisi Zacharia Samson wa Dinari ya Chato amesema Umasikini ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya kihuduma ambapo amesema mafunzo hayo ya CCMP yamekuja kwa wakati muafaka ambao kanisa na jamii linayahitaji.

Mratibu wa Ushirika wa Wamama wa Kikristo wa Anglikana Tanzania Kanda ya Ziwa Judith Kaigarula amesema ni vizuri waliopata mafunzo hayo kwenda kuyafanyia kazi ili watu wazijue Rasilimali na fursa za kiuchumi ili wakazifanyie kazi kwa lengo la kujiendeleza kiuchumi.

“umasikini unachangia kwa kiwango kikubwa hata kazi ya Mungu kutofanyika vizuri kutokana na wakristo kushindwa kuwa na fedha hata kutoa sadaka kwenye ibada”, amesema

Askofu wa Kanisa Angalikana Tanzania, Dayosisi ya Biharamulo mkoani Kagera, Vithalis Yusuph akiteta jambo na Katibu wa Ushirika wa Wamama wa Kikristo Tanzania (UMAKI), Canon Dkt. Margareth Ndonde wakati wa ufunguzi wa warsha ya CCMP Mkoani Kagera







Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG