BANDA MEDIA BLOG

FINISH DC SHEKIMWERI NA VIJANA WA GEN - S WAHITIMISHA MBIO ZA POLE ZA KM 6

 

NA JOHN BANDA, DODOMA

MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabiri Shekimweri amewaasa vijana wa Kizazi cha Mafanikio (GEN-S) kutumia muda wao mwingi kufuatilia yanayoendelea katika nchi kwa utekelezaji wa serikali iliyopo madarakani badala ya kupoteza Muda kwa mambo yasiyo na faida.

 Shekimweri ameutoa wito huo katika uwanja wa jamhuri jijini Dodoma mara baada ya kukamilika kwa mbio za pole za kilometa 6, zilizoambatana na mazoezi ya viungo zilizoandaliwa na GEN-S zikiwashirikisha vijana kutoka katika makundi mbalimbali wakiwemo wa vyuo vikuu.

"kwa sisi tunaopata nafasi za kufanya usaili wakati mwingine unashangaa unamuuliza kijana ambaye ni mhitimu kabisa wa chuo kikuu, swali  dogo tu,  kama nini kifupi cha treni ya mwendo kasi inayotumia umeme unaona anaangalia chini hana jibu", amesema

amesema Tanzania ina Miradi mikubwa inaendelea vijana wafatilie ili kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu nchi yao ili inapotokea fursa wanaitumia wakiwa wanajua cha kufanya.

kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara Sanaa, Utamaduni na  michezo  Cosmas Tamba amewaagiza Maofisa Michezo wa Mikoa, kuhakikisha wanavisaidia vilabu vya  Jogging kufanya usajili ili iwe rahisi kufanya michezo yao kwa utaratibu huku wakishirikiana kwa karibu na serikali.

"maofisa michezo wa mikoa hakikisheni vilabu vya jogging vyote vinasajiliwa, pia viongozi wa vilabu hivyo tengenezeni katiba na miongozo yenu  ili mfanye vizuri katika shughuli zenu za michezo", amesema












Mwanamuzi wa miondoko ya Singeli Dullah Mkabila akiwapagawisha vijana wa GEN-S Katika uwanja wa jamhuri jijini Dodoma

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG