Ukiwa barabara mwisho wa kila mwaka utaona magari mapya na madereva wapya kwenye safari za masafa wakiendesha bila kufata ALAMA za BARABARA ipasavyo huku wakiwa hawana utulivu barabarani
JAMBO LINGINE NI FATIGUE safari ya masafa marefu inahitaji utimamu wa mwili na maandalizi ya safari za masafa marefu
Unakuta mtu ni mhasibu HR au mfanyabiashara miaka yote yupo ofisini udereva wake ni ofisini na nyumbani
Mwisho wa mwaka anachukua familia nzima anaendesha kutoka Dar es Salaam hadi Bukoba Mwanza Arusha Mbeya nk
Mwishoni mwa mwaka kuna mamia ya madereva wa aina hii huko njiani wanakula vyakula ovyo ovyo na kunywa vinywaji.
KWA UFUPI
ELIMU KUBWA YA ESSENTIAL DEFENSIVE DRIVING SKILLS inatakiwa kutolewa itasaidia wengi kuacha kuingiza mamia ya magari kuelekea mikoani bila kufata MIIKO SHERIA NA TARATIBU ZA UENDESHAJI WA MAGARI KWENYE BARABARA ZA MASAFA MAREFU.
