▪️Washiriki Bonanza la Michezo na Askari Magereza
▪️Watoa misaada mbalimbali kwa wafungwa
▪️Wafanya ukarabati wa Jiko lq
chakula kwa Wafungwa wanawake
▪️Jeshi la Magereza lapongezwa kwa matumizi ya Nishati Safi
................
📍Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde, ametembelea Gereza Kuu Isanga akiambatana na wadau wa maendeleo Dodoma, maarufu kama 'Dodoma Legends' jana Desemba 28, 2024 na kupokewa na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza (CP) Nicodemus Tenga kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania (CGP) Jeremiah Katungu.
Katika ziara hiyo CP Tenga amepokea zawadi za vitu mbalimbali kutoka kwa Waziri wa Madini na Mbunge wa Dodoma Mjini.
Kamishna Nicodemus Tenga amemshukuru Mhe. Mavunde pamoja na wadau alio ambatana nao kwa kuamua kutembelea Gereza la Isanga na kutoa zawadi mbalimbali kwaajili ya matumizi ya Wafungwa
na Mahabusu huku akisema hiyo ndio namna bora ya ushirikishwaji wa
