BANDA MEDIA BLOG

Tsunami ya 2004: Miaka 20 baadaye, nchi kadhaa za Asia zaomboleza vifo vya raia wao

 

Moja ya barabara katika Phuket iliyoharibiwa na tsunami, Desemba 26, 2004. AP - KARIM KHAMZIN

Kutoka kwa mwanahabari wetu nchini Thailand,

Nchini Thailand, ambako nusu ya watu zaidi ya 5,000 waliokufa walikuwa watalii wa kigeni, maombolezo yasiyo rasmi yalitarajiwa kufuatia hafla ya ukumbusho ya serikali. 

Kumbukumbu kwenye fukwe na ibada za kidini zitafanyika kote Asia, hususan IndonesiaSri LankaIndia na Thailand, ambazo ndizo zilizoathirika zaidi. 

Mnamo Desemba 26, 2004, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 9.1 karibu na ncha ya magharibi ya Indonesia lilisababisha mawimbi makubwa yaliyopiga pwani za nchi 14 kuanzia Indonesia hadi Somalia.

Indonesia ilipoteza watu zaidi ya 160,000, ikiwa ndiyo iliyoathirika zaidi. Katika mkoa wake wa magharibi wa Aceh, waombolezaji walikusanyika kwa dakika ya ukimya, kisha kutembelea kaburi la pamoja na kufanya sala ya kijumuiya katika msikiti mkuu wa mji mkuu wa mkoa huo, Banda Aceh. 

Nchini Sri Lanka, ambapo zaidi ya watu 35,000 walifariki, manusura na jamaa walikusanyika kuwakumbuka takriban waathiriwa 1,000 waliokufa wakati mawimbi yalipogonga treni ya abiria na kuiondoa kwenye reli.

Karibu watu 300 walifariki katika nchi ya mbali ya Somalia, zaidi ya 100 katika Visiwa vya Maldives, na kadhaa nchini Malaysia na Myanmar

Janga hili kubwa la tsunami liligharimu maisha ya watu 220,000 na kuharibu maeneo ya pwani ya Bahari ya Hindi, likiwa moja ya majanga makubwa zaidi katika historia ya binadamu.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG