BANDA MEDIA BLOG

Wafuasi wa Assad watafutwa kwa udi na uvumba baada ya makabiliano makali huko Syria

 

Kulingana na shirika lisilo la kiserikali la SOHR, serikali mpya ya Syria ilitaka kumkamata mmoja wa viongozi wa utawala wa zamani wa Assad huko Tartous, wakati makabiliano yalipozuka. Hapa, taswira ya angani ya jiji la bandari la Tartus, magharibi mwa Syria, tarehe 18 Desemba 2024. © Omar Haj Kadour / AFP

.......................

Na:


Operesheni hiyo inafanyika katika mkoa wa pwani wa Tartus (magharibi), ngome ya walio wachache kutoka dhehebu la Alawite ambako rais aliyeondolewa madarakani anatoka Assad aliotimuliwa mamlakani tarehe 8 Desemba na muungano wa waasi unaoongozwa na kundi la Waislam wenye itikadi kali la Hayat Tahrir al-Sham (HTS) .

Operesheni hii imefanya iwezekane "kuangamiza idadi fulani" ya  "wanamgambo" watiifu kwa Bashar Al Assad, linabainisha shirika la habari la serikali SANA. Lengo ni "kurejesha usalama, utulivu na amani ya raia" katika eneo hili la pwani, linabainisha shirika hili la habari.

Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu la Syria (SOHR) limeripoti "vifo vitatu" katika operesheni hii, na kubainisha kuwa waathiriwa ni kutoka safu ya "wapiganaji watiifu kwa serikali ya zamani".

- Watu kadhaa wakamatwa -

Shirika hili lisilo la kiserikali lenye makao yake makuu nchini Uingereza, ambalo lina mtandao mkubwa wa vyanzo nchini Syria, pia limeripoti "kukamatwa" kwa watu kadhaa kuhusiana na mapigano na maandamano ya watu kutoka dhehebu la walio wachache la Alawite siku moja kabla.

Kulingana na mashahidi na SOHR, maelfu ya Wasyria walifanya maandamano siku ya Jumatano huko Tartus, Banias, Jableh, na Latakia magharibi mwa nchi, ambapo jamii ya Alawite, tawi la Uislamu wa Kishia, iko, na pia huko Homs (katikati), baada ya kurushwa video inayoonyesha shambulio dhidi ya moja ya sehemu zao takatifu.

Maandamano haya ni ya kwanza tangu kupinduliwa kwa bwana Assad.

"Mwandamanaji mmoja ameuawa na watano wamejeruhiwa baada ya vikosi vya usalama huko Homs kufyatua risasi kuwatawanya waandamanaji," kulingana na SOHR.

Watu kutoka jamii ya Alawite walipandwa na hasira baada ya kurushwa video kwenye mitandao ya kijamii inayoonyesha "shambulio la wapiganaji" dhidi ya sehemu takatifu ambayo ilichomwa moto huko Aleppo (kaskazini), kulingana na SOHR. Wafanyakazi watano wa sehemu hiyo katifu waliuawa, kulingana na shirika hili lisilo la kiserikali.

Huko Damascus, Wizara ya Mambo ya Ndani imehakikisha kuwa video hiyo ni "ya zamani" na ni ya tarehe ya kutekwa kwa Aleppo na waasi mnamo Desemba 1.

"Lengo la kusambaza tena picha kama hizo ni kuzusha mifarakano kati ya raia wa Syria (...)," wizara imeongeza, ikishutumu "makundi yasiyojulikana" yaliyofanya shambulio hilo.

Hata hivyo, makabiliano kati ya watu wenye silaha na vikosi vya usalama ambao walikuwa wakijaribu kumkamata afisa wa serikali iliyoondolewa katika jimbo la Tartous yalisababisha vifo vya watu 17 siku ya Jumatano, kulingana na SOHR.

Wakati wa makabiliano haya, "wajumbe kumi na wanne wa Wizara ya Mambo ya Ndani waliuawa na wengine 10 kujeruhiwa," Waziri mpya wa Mambo ya Ndani Mohammed Abdel Rahman amesema katika taarifa.

Kulingana na SOHR, watu watatu waliokuwa na silaha pia waliuawa.

- "Hali inaweza kuwa mbaya zaidi" -

Mamlaka mpya zimeongeza ishara za uhakikisho kwa watu wote walio wachache katika nchi iliyoathiriwa na miaka 13 ya vita vikali, vilivyoanzishwa mwaka 2011 na ukandamizaji wa kikatili wa maandamano ya kuunga mkono demokrasia, na ambayo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 500,000.

Huko Jableh, waandamanaji waliimba "Alawite, Sunni, tunataka amani", muandamanaji, Ali Daoud, ameliambia shirika la habari la AFP, akitaka "wauaji waadhibiwe".

Picha zimeonyesha umati wa watu wakiandamana mjini, wakipeperusha bendera ya waasi enzi za uhuru.

"Hapana kuteketeza kwa moto mahali patakatifu na ubaguzi wa kidini, ndio kwa Syria iliyo huru," imeandikwa kwenye moja ya mabango.

"Kwa sasa tunasikiliza wito wa utulivu (...) Lakini hali inaweza kuwa mbaya zaidi," amehofia Ghidak Mayya, muandamanaji mwenye umri wa miaka 30, huko Latakia.

Baada ya Bashar Al Assad kukimbilia Moscow kutokana na mashambulizi ya waasi, wanachama wa wachache wa Alawite walifurahia kuanguka kwake lakini walisema wanahofia kutengwa au kulipizwa kisasi.

Kulingana na mtaalamu wa masuala ya siasa Fabrice Balanche, "Alawite walikuwa karibu sana na utawala wa Bashar", ambao waliunda "kikosi cha walinzi wa rais". Anakadiria idadi yao kuwa milioni 1.7 leo, au karibu 9% ya raia.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG