BANDA MEDIA BLOG

Mashirika ya kiraia kuwasilisha suala la utekaji nyara mbele ya mahakama za kimataifa

 

Maafisa wa polisi wanamkamata mwanamume mmoja mjini Nairobi, Kenya.
Maafisa wa polisi wanamkamata mwanamume mmoja mjini Nairobi, Kenya. REUTERS - Monicah Mwangi

Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Gaëlle Laleix

Mashirika hayo mawili yanataka mahakama nchini Kenya itambue kuwa utekaji nyara unaotekelezwa na polisi unawakilisha uhalifu dhidi ya ubinadamu. Kulingana na mwanasheria wao, Wakili John Khaminwa, “Ibara ya 7 ya Mkataba wa Roma inazingatia kwamba kitendo cha watu kutekwa na kutoweka, kinapotumiwa kama chombo cha kisiasa cha ukandamizaji, ni uhalifu. "

Kwa upande mwingine, mashirika hayo mawili yanashutumu Polisi wa taifa wa Kenya kwa kutokuwa na uwezo wa kuchunguza utekaji nyara huu. "Mkuu wa polisi mwenyewe alikiri, (wiki iliyopita) ni wazi kwamba polisi wanashindwa katika kutekeleza majukumu yao" inahitimisha taarifa yao kwa vyombo vya habari.

Hali mbaya iliyokithiri

Kwa mujibu wa Gacheke Gachihi, mratibu wa Kituo cha Mathare kwa ajili ya Haki ya Kijamii, utekaji nyara wa washawishi sita kwenye mkesha wa Krismasi ni hali mbaya ambayo imekithiri. “Tumekuwa tukirekodi visa vya watu kutoweka, uhalifu unaofanywa na polisi kwa zaidi ya miaka kumi na hakuna kilichobadilika. Ni tatizo la kimfumo,” anabainisha.

Mkuu wa polisi na katibu wa baraza la mawaziri la Wizara ya Mambo ya Ndani waliitwa na mahakama mnamo Januari 8 kuripoti kuhusu hatima ya wale waliotoweka mkesha wa Krismasi.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG