wa Hamas ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kundi hilo "limekubali kuwaachilia wafungwa 34 wa Israel kutoka kwenye orodha iliyotolewa na Israel katika awamu ya kwanza ya mpango wa kubadilishana wafungwa." Orodha hii, ametaja, inajumuisha "wanawake wote, wagonjwa, watoto na wazee" kati ya mateka wa Israeli.
"Hamas na makundi ya upinzani yanahitaji takriban wiki moja ya utulivu kuwasiliana na wateka nyara na kutambua (mateka) waliofariki au walio hai," ameongeza afisa huyo, ambaye ameomba kutotajwa jina. Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu imesema katika taarifa yake kwamba "kinyume na ilivyoripotiwa, Hamas bado haijatoa orodha ya mateka."
Hakuna mapatano yanayowezekana tangu Novemba 2023
Mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Hamas na Israel yalianza tena mwishoni mwa juma hili nchini Qatar, kwa nia ya makubaliano ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa huko Gaza tangu shambulio la vuguvugu la Wapalestina katika ardhi ya Israel mnamo Oktoba 7, 2023.
Licha ya juhudi kubwa za kidiplomasia zilizoongozwa chini ya uangalizi wa Qatar, Misri na Marekani, hakuna mapatano yaliyohitimishwa tangu yale ya wiki moja mwishoni mwa mwezi wa Novemba 2023, ambayo yaliwezesha kuachiliwa kwa mateka 105 badala ya wafungwa 240 wa Kipalestina wanaoshikiliwa na Israeli. . Duru hii mpya ya majadiliano huko Doha inakuja zaidi ya wiki mbili kabla ya kuapishwa, Januari 20, kwa Rais mteule wa Marekani Donald Trump, ambaye tayari ameweka shinikizo kwa Hamas.