Waziri wa Afya, Jenista Mhagama akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) jijini Dodoma leo Januari 21, 2025, ikiwa ni iashara ya uzinduzi rasmi wa bodi hiyo.
....................
Mhagama akiwa na wajumbe wa bodi hiyo baada ya kuwakabidhi vitendea kazi.

WAZIRI wa Afya Jenista Mhagama ameitaka Bodi mpya wa kurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kushugulikia Maslahi ya watumishi ili iwe rahisi kudai wajubu katika utendaji wao
Mhagama ametoa Agizo hilo wakati alipokuwa akizindua Bodi mpya ya Afya NHIF uzinduzi uliofanyika, jijini Dodoma ambapo ameongeza kuwa bodi hiyo inatakiwa kuwa wazi kwa kuwashirikisha wananchi katika mipango wanayoifanya wahakikishe wanawakumbuka na kuwajali wananchi wa hali ya chini. Pia ameagiza kutomuonea haya mtumishi yeyote atakayeharibu taswira nzuri ya Taaisi hiyo.
Mhagama akiwa na wajumbe wa bodi hiyo baada ya kuwakabidhi vitendea kazi.
Baadhi ya wajumbe wa bodi.
Tags
AFYA