Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameongoza kikao cha Kamati ya Uongozi kilichopokea na kujadili Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge tarehe 27 Januari, 2025 Bungeni Jijini Dodoma.
Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge unategemewa kuanza tarehe 28 Januari, 2025 Bungeni Jijini Dodoma.
Vile vile Waheshimiwa wajumbe wa kikao hicho walisimama kwa dakika moja kama ishara ya kumuombea Marehemu Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mkuu Mteule wa Shirikia la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika aliyefariki Dunia tarehe 27 Novemba 2024.
Tags
BUNGE TANZANIA









