BANDA MEDIA BLOG

SERA MPYA YA ELIMU KUZALISHA WANAFUNZI WENYE MAARIFA,MAADILI NA UJUZI NCHINI

 

KATIBU  Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw.Gerson Msigwa,akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 29,2025 kuelekea katika uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 yenye lengo la kuleta mageuzi ya utoaji elimu nchini unaotarajiwa kuzinduliwa Januari 31,2025 jijini Dodoma na Rais Samia Suluhu Hassan.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo,akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 29,2025 kuelekea katika uzinduzi huo unaotarajiwa kuzinduliwa Januari 31,2025 jijini Dodoma na Rais Samia Suluhu Hassan.

DODOMA

KATIBU  Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw.Gerson Msigwa,amesema Sera Mpya ya Elimu inakwenda kuzalisha  wanafunzi wenye maarifa, maadili na ujuzi utakaowawezesha wahitimu kwenye ngazi mbalimbali kujiajiri na kuajiri wengine na kuongeza uwezo wa ushindani kwenye soko hilo.

 Bw.Msigwa,ameyasema hayo  Januari 29,2025  wakati akizungumza na waandishi wa habari  kuelekea katika uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 yenye lengo la kuleta mageuzi ya utoaji elimu nchini unaotarajiwa kuzinduliwa Januari 31,2025 jijini Dodoma na Rais Samia Suluhu Hassan.

Bw.amesema kuwa lengo la kufanyiwa mapitio hayo ya sera ni kuwafanya wanafunzi kuwa na umahiri na ujuzi unaoakisi mahitaji kitaifa na kimataifa ili kushindana na kushiriki kikamilifu kwenye soko la ajira duniani.

“Miongoni mwa mageuzi yaliyopo kwenye sera hiyo ni kufundishwa kwa somo la Tehama, mafunzo ya ufundi stadi kuanzia elimu ya msingi na matumizi ya akili unde(AI).”amesema Bw.Msigwa

Aidha amesema  sera hiyo itazalisha wanafunzi wenye maarifa, maadili na ujuzi utakaowawezesha wahitimu kwenye ngazi mbalimbali kujiajiri na kuajiri wengine na kuongeza uwezo wa ushindani kwenye soko hilo.

“Mapitio hayo yanaendana na utekelezaji wa Ilani ya CCM kuhusu kuimarisha huduma za kijamii ambapo imejielekeza kuhakikisha kila rasilimali watu inakuwa na ujuzi,”amesema 

Hata hivyo ameeleza  kuwa mapitio hayo yameshirikisha wadau na matokeo makubwa yanatarajiwa kwa kuwa huduma ya elimu inagusa moja kwa moja jamii.

Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo amesema  sera hiyo itazinduliwa sambamba na vitendea kazi ikiwamo mkakati wa utekelezaji wa sera ambao tayari umeandaliwa.

“Sera hiyo ilielekeza kuboresha mitaala ya elimu ambayo imeboreshwa kwa ngazi zote kuanzia ngazi ya awali na vyuo vikuu kwasasa vinaendelea kuboresha.”amesema Prof.Nombo

Aidha amesema  kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia, sekta ya elimu kupitia sera hiyo umeandaliwa mkakati wa matumizi ya Tehama katika kujenga uchumi wa kidigitali.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG